Katika kukuza utalii, tutumie wageni wa kimataifa kutangaza vivutio vyetu

Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
270
563
Wana JF,

Hivi katika kukuza na kujitangaza ktk utalii wetu hasa kwa watu wa nje, wa ndani nitarejea tena itakuwa topic inayojitegemea.

Hivi ni vigumu sana kuwasiliana na Club kubwa kubwa duniani zenye mashiko ktk nyaza/ medani za kimichezo zinazo tazamwa zaidi duniani kuwashawishi waje wapate mapumziko kidogo hata pale Serengeti na viunga vyake tukazidi kutengeneza headlines duniani na hapo naona kama tutakuwa tumefanya jambo flan (Ikumbukwe najaribu kutoa general view, mikakati kwa jinsi gani Wahusika wapo wanaweza ona mbali zaidi na kujua nini wanaweza fanya).

Pia wageni Mashuhuri wanaotutembelea kwa shughuli mbali mbali katika Taifa letu, Wakiwasili wapelekwe japo kwenye ma-snake park hivi hii itazidi kutuwakilisha vema huko nje yaani kila mgeni mashuhuri akija tunatumia fursa kujitangaza kwenye nyanja za kitalii kimtindo flan hivi very technically!

Watumishi wa MUNGU katika nyanja zote za dini (Dini zote) wakaungana kwa pamoja wakawa na trip tour za pamoja kutembelea moja ya vivutio vikubwa kwa vidogo kwanza wakitambulisha Tanzania ni nchi yenye Amani, upendo na yenye vivutio adimu na watu wake ni wakarimu sana.

Wakiwa huko pia wanapiga na dua/maombi kwa Taifa letu ili Taifa letu lizidi kudumisha amani, upendo, mshikamano na liwe Taifa lenye hali ya kupenda kufanya kazi na kuwajibika kwa mujibu wa sheria, Pia liwe Taifa lenye kumtumaini MUNGU pia katika nyanja tofauti tofauti.

Viongozi wetu pia wapate kamda kidogo kutembelea siyo tu mpaka uzinduzi fulani fulani.

Ongezeni mawazo.

Naamini wachangiaji wana mawazo mazuri pia karibuni.

#KwaFaidaYaTaifaLetu
#MawazoChanya
View attachment 1761231View attachment 1761230
 
Ukizungumzia watu mashuhuri na vilabu vikubwa tayari hayo ni matangazo sasa kwa nini tusiwe na mpango mkakati ulio endelevu wa sisi kuwa mabalozi badala yakutegemea kuwa wao ndiyo watakuwa wanatutangaza. Niishie hapo maana kuna kitu kinapikwa.
 
Pia Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza landing fees kwa mashirika ya ndege.

Jomo Kenyatta airport landing fees zao ni nafuu ndio maana ndege nyingi zinatua pale na kuwabakiza watalii wengi zaidi.

Tanzania tuna vivutio vingi vya utalii lakini hatupo serious kwenye kuvutia watalii ambao wanalipa nauli za ndege ghali zaidi ikiwa ndege inatua KIA .
 
Ukizungumzia watu mashuhuri na vilabu vikubwa tayari hayo ni matangazo sasa kwa nini tusiwe na mpango mkakati ulio endelevu wa sisi kuwa mabalozi badala yakutegemea kuwa wao ndiyo watakuwa wanatutangaza. Niishie hapo maana kuna kitu kinapikwa.
Asante kwa mawazo yako, umechangia vema. safiiiii
 
Hatujachelewa mpaka muda huu tuje na sera itakayoishi vizazi na vizazi itakayo kuwa shindani kuanzia ndani na njeya mipaka yetu mpaka kimataifa na jinsi ya kuipa vipaumbele vivutio vyetu kwanza na hii iende sambasamba na uzalendo kwa kila mtu mmoja mmoja ajione ana chumba chake cha mafanikio katika hili taifa asiwepo mtu amebaki nyuma labda ni jukumu la mtu fulani isipokuwa kila mtu analo jukumu lakuwa balozi wa kuliongelea taifa vyema na pia vivutio vyake.
 
Upo Sahihi mkuu, Ila kwa akili za Serekali ya CCM wanahisi Zuchu ndie atachochea kukua kwa utalii, unakuta nae ni Balozi wa Utalii
 
Back
Top Bottom