Katika hili, jiji la Mwanza halina budi kujifunza kwa Bunda

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Ndugu zangu wana Mwanza hata kaka mkubwa pia ujifunza kwa wadogo zake na siyo vibaya kuiga kizuri ikiwa mwenzio kafanya na kufanikiwa.

Mji wa Bunda ni moja ya miji mizuri kimandhari na mwonekano kwa sasa Tanzania kwa wale wanaosafiri na kufanya utalii wa ndani watakubaliana nami,

Mji huu unaozidi kukua kila kukicha awali ulikuwa ukishika nafasi ya tatu tena ukiwa mji mdogo nyuma ya mji wa Tarime lakini bila shaka hivi sasa ndiyo mji wa pili baada ya Musoma na hata hivyo Musoma pia ni kama inawashiwa indicator ikae mguu sawa maana mji huu kwa sasa umezidi kuimarika zaidi kimiundombinu,biashara na utalii.

Mji huu wenye safu ya milima ya hifadhi ya taifa ya Balili pamoja na hifadhi ya taifa ya Serengeti huku upande wake mwingine ukiwa umezingirwa na mandhari nzuri ya ziwa Victoria inayosindikizwa na ujenzi mzuri wa makazi ya kisasa yaliyopangiliwa.

Kuna mandhari nzuri ya miti ya asili na barabara nzuri zenye upana wa kutosha na zenye taa zinazofanya kazi pamoja na hali nzuri ya usafi uifanya Bunda kuvutia ajabu kwa nyakati zote iwe ni usiku ama mchana.

Hivyo basi mji huu umwacha mgeni na experience kubwa sana ambayo wenda akutegemea kama angeipata kwa kutembelea mahali hapa ukilinganisha na miji mingine mikubwa kama Mwanza iliyozubaa.

Je, kwanini nimewataka wana Mwanza wasione aibu kuiga mazuri ya mji wa Bunda?

Mji wa Bunda umehifadhi mazingira yake kiasili na umejua namna ya kutumia mandhari yake ya asili ya safu ya mlima Balili kuvutia utalii kwa kujenga hoteli nzuri juu ya kilele cha mlima huu (pongezi kwenu landmarks hotels na halmashauri ya wilaya) kwa ubunifu huu wa aina yake na wa mara ya kwanza kwa Tanzania.

Bunda ndiyo mji pekee unaoweza kuketi mtaani kwako umbali wa kilomita moja na ukatizama game ya simba na yanga katika screen kubwa mlimani lakini pia ukifurahia mandhari ya mnyororo wa taa na led zilizopamba kilele cha mlima huo nyakati za usiku na usiamini kama huko wilayani.

Mwanza ilikuwa na potential kubwa kuliko hii iliyonayo Bunda cha ajabu wakakimbilia milimani kujenga makazi holela na ya ovyo bila ya vyoo na matokeo yake mji ukaishia kuwa na sura mbovu.

Lakini siku zote kuteleza si kuanguka bangosha ningeomba walahu na ninyi muige japo mweke vi-taa taa vya urembo wa mchongo juu ya safu ya milima chungu nzima iliyopo Mwanza walahu nyakati za usiku kuwepo na mandhari nzuri ukizingatia hata taa za kuweka mji safi pia ni tatizo.

NB: Si kwa Mwanza tu bali miji yote Tanzania yenye mandhari nzuri ya milima mirefu, na misitu jitahidini kuiga mazuri kama haya hili Tanzania yetu iwe ni sehemu nzuri yakuvutia.
 
Back
Top Bottom