Serikali imefanya maamuzi ya kupeleka madaktari zaidi 500 waliomaliza masomo na internship lwakaajiliwe kenya kwa kuwa serikali haina uwezo kuajili kwa sasa na si kwa sababu hatuna maitaji!!! Moja ya changamoto kubwa ya vituo vya afya, zahanati& hospitali ni uhaba wa madaktari! vijijini hali ni mbaya sana kiasi kwamba zahanati nyingi zinahudumiwa na manesi , au ma clinical officer nao! Chuzi tu, tumeona wananchi wakiandamana kwa kushinikiza kuhamishwa kwa wauguzi waliogoma kuamka kumsaidi mama mjamzito aliyekuwa tayari kujifungua,,,,kwa kuwa walikuwa hawapo zamu usiku!! Mimi najiuliza ni nini kipaumbele cha serikali ya sasa kama si afya? Ni kweli serikali haoni umuhimu wa kuwa na madaktari wa afya kwa kuwa watanzania tumezoea kukaa masaa 10 tukisubiri dk mmoja atuhudumie watu zaidi 300 kwa masaa 8, na baada hapo unaporudi na vipimo unakuta daktari wa mwanzo ameondoka kwa hiyo dawa anakuandikia daktari mwingine!!! Ni kipaumbele gani muhimu kinachozidi afya watanzania?? Mungu atusaidie ikiwa madaktari hawaajiliwi basi kwa wengine ni giza tupu!