Katika Elimu, Tanzania tunazidi kufeli.

Kijana Mzeeeh

JF-Expert Member
Jul 1, 2015
295
324
Nashindwa kuielewa Serikali katika swala la kuwapangia shule wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha tano.

Madogo wana-loose tu mtaani huku. Mtoto amemaliza mtihani wa kidato cha nne mwaka jana Novemba, na matokeo yametoka tangu mwishoni mwa mwenzi Januari mwaka huu, lakini hadi leo yupo tu. Anasubirishwa karibu nusu mwaka kupangiwa shule ya kwenda. Nikikumbuka kipindi chetu sisi, muda kama huu, tumesha anza masomo.

Tunajitahidi kuwatafutia vikozi kozi ata vya Computer ili kupunguza hasara ya kukaa muda mrefu bila shughuli kwenye akili na tabia zao, vikozi wanavimaliza lakini allocations bado! Matokeo yake wanakaa mitaani wana anza na vitabia vya ajabu ajabu ambavyo havifai kwa mwanafunzi.

Baadhi ya shule binafsi zimesha anza masomo tangu mwezi uliopita, harafu tunategemea wadogo zetu wanaosubiri kupangiwa shule za serikali waje kushindana nao katika mtihani wa kidato cha sita. Mtoto amechelewa kuanza masomo na anaweza fika shuleni walimu wasitoshe.

Mdogo wangu ananiuma sana natamani ata nikapige dili haramu nimpeleke shule binafsi, nahisi anapotea kabisa ukidhingatia ni wa Kike. Kwani hizi shule binafsi hazishikiki, karo utafikiri unanunua Gari.
 
Back
Top Bottom