Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini China Alawi Abdallah amesema Watanzania wote walioko nje ya nchi ambao wamekuwa wakilalamikia mifumo ya uchaguzi na demokrasia nchini Tanzania wamekuwa hawana dhamira ya dhati ya kutaka mabadiliko bali wamekuwa wakiongoza na maslahi binafsi na chuki binafsi kwa baadhi ya Viongozi na Vyama vya siasa vilivyoko nchini Tanzania.
Alawi ametoa kauli hiyo wakati wa Mdahalo wa pamoja ulioandaliwa jijini Dar es Salaam na kuhusisha Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu nchini, akitolea mfano kwa baadhi ya Watanzania wanaoishi kwenye nchi zenye mfumo wa Malkia na Mfalme na bado wamekuwa wakilalamikia mfumo wa uchaguzi nchini na vile ambavyo chaguzi zimekuwa zikifanyika