Katibu wa CHADEMA Mbeya anaswa kwa rushwa

Katibu wa CHADEMA Mbeya anaswa kwa rushwa

Hapo takukuru wanaona wamefanya kazi kubwa kumbe ni siasa tu
 
Anyongwe huyo anapenda pesa za njia fupi
 
Ni mambo ya nyakati kwa anayekumbuka ghiriba na mateso ya gadhaf kwa wapinzani wakeLibya kwa kushindwa kutambua nyakati

na mabadiliko kilichomkuta ilikuwa mjukuu. NI nyakati na mabadiliko ambavyo ccm inajitahidi kupingana navyo wakisahau kwamba

wakati na mabadiriko ya kinyakati hayapingiki kwa mbinu na mikakati ya aina yoyote ile ..........
 
Tafuta visababu hata vya mke wa kiongozi wa CDM kata lakini mjue kwamba M4C with no apologize.
 
Habari takataka tu hiyo kwan mmeshindwa kudhibiti fedha za Richmond alafu mje na skendo ya 73000 tena vihera vyenyewe hata mke hupewi. Habari za kijuha kabisa hizi nyie magamba.
 
Anyongwe huyo anapenda pesa za njia fupi


Mimi ningependa sana wahalifu na hasa wa rushwa wanyongwe wote ilitufaidi haki zetu.

Tatitizo watanyongwa walalahoi tu wa vijihela vya kununulia baiskeli lakini wezi halisi na wanaotusababishia umaskini wetu

wataendelea kula bata kila siku. Hatuwaoni akina mramba, Yona, Rostam au wazee wa Richmond hapa imekaaje?
 
watanzania tuna utamaduni wa rushwa.
kujaza fomu ni elfu sitini mpaka laki moja mahakamani ..... kujaZA FOMU TU, NA risiti hupati.
Nikawauliza za nini? wakaniambia za chai...live!!
Nikawatishia kuwa namjua jaji fulani, kwa hiyo acheni hizo ... wakaniambia sasa hivi kuna foleni njoo baada ya two weeks.
hakuna cha CDM, CCM, CUF wala TLP ...watanzania tuna utamaduni wa rushwa!!
 
Imeandikwa tarehe 05 Desemba 2012 | Mwandishi wa HabariLeo

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) James Mpalaza wa Wilaya ya Mbeya Vijijini amenaswa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) akipokea rushwa ya Sh 73,000.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa, Mpalaza ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Ardhi katika Kata ya Nsalala alidai rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ahadi Ndile kwa lengo la kumpatia hukumu iliyotolewa na Baraza hilo.

Ndile alikuwa kwenye mzozo wa mpaka na Diwani wa Kata ya Ikukwa Viti Maalumu, Monica Degua (CCM) na Baraza hilo lililopo Mbeya vijijini lilimpa ushindi Degua. Ndile alithibitisha kutokea tukio hilo akisema;

“Sikuridhishwa na hukumu ya Baraza, nikaamua kuomba nakala ya hukumu ili nisonge mbele, mwanzo waliniambia nipeleke Sh 10,000 ili niandikiwe taarifa nzuri sana.

“Nilipokwenda na fedha hizo ambazo walidai ni gharama za Barazahttp://en.wikipedia.org/wiki/Fair_trade, walidai hazitoshi na nitapewa endapo tu nitapeleka Sh 73,000. Sikuona sababu ya kupeleka fedha hizo ndipo nilipowasiliana na Takukuru ambao leo (jana) wamefanya kazi yao,” alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya, Daniel Mtuka alikiri kumshikilia Mpalaza kwa tuhuma hizo kwa pamoja na
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Asia Haruna.

Akizungumzia tukio hilo alisema Novemba 26 mwaka huu ofisi za Takukuru mkoani hapo zilipata taarifa kutoka kwa mlalamikaji aliyefahamika kwa jina la Ahadi Ndile ambaye alikuwa na kesi ya madai namba 26, 2012 ya kugombea mpaka yeye na jirani yake Monica Degula.

Alisema kutokana na mgogoro huo wa mpaka, walipeleka kesi katika Baraza hilo ambapo baada ya uamuzi, Ndile alishindwa na Monica na hakuridhika na uamuzi huo na hivyo kuamua kuomba kupatiwa mwenendo wa shauri pamoja na hukumu.

Mtuka alisema wakati akiomba kupatiwa hukumu hiyo ndipo alipotakiwa kuhonga Sh 73,000 kwa Mpalaza ambaye ni Katibu wa Baraza hilo ikiwa ni pamoja na Sh 10,000 kwa ajili ya gharama ya kesi.

Hata hivyo Mtuka alisema migogoro ya ardhi imekuwa kero katika eneo hilo na kwamba Takukuru ina majalada mengi yatokanayo na malalamiko kutoka kwa wananchi wakitakiwa kutoa rushwa na kudhulumiwa haki zao.

Alisema bado wanahojiana na Ndile pamoja na Mwenyekiti lakini aliyepokea fedha hizo ni Mpalaza.
wewe kumbe ni maamuzi ya baraza ona kwanini huyoasia haruna hawamtaji wazi nahisi gazeti hili ni la akina chichidodo(mangula) magamba hayoooo na gazeti lao
 
Chamsingi siyo gazeti gani limeripoti bali iwapo habari hizo ni za kweli au la. Gazeti la tanzania daima liliripoti habari za mbunge wa bahi kupokea na kukamatwa kwa rushwa. Je habari hizo zingebezwa ati kwa sababu gazeti hilo ni la chadema? Let us call a spade spade and not big spoon. Uzinzi ni uzinzi tu hata kama kafanya shetani au nabii.
 
Njaa mbaya sana na cdm kazi ipo maana wengi wanajiunga wakifikiria kuna hela lakini tusirudi nyuma tukaze boot tu hadi kieleweke
 
Kweli hosea na timu yake ni wachumia tumbo

ile rushwa iliyofanyika kwenye chaguzi za ccm kule dodoma kwenye mkutano wao huu ulioisha hivi majuzi hawakuziona??hizi propaganda zingne ni za kitoto sana
 
Back
Top Bottom