Katibu wa CHADEMA Mbeya anaswa kwa rushwa

Katibu wa CHADEMA Mbeya anaswa kwa rushwa

Kama ametenda kosa hilo sheria ichukue mkondo wake na CDM ichukue hatua stahiki tena ikiwezekana andikiwe barua ya kujieleza mapema hii ni kuonyesha uwajibikaji
 
Imeandikwa tarehe 05 Desemba 2012 | Mwandishi wa HabariLeo

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) James Mpalaza wa Wilaya ya Mbeya Vijijini amenaswa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) akipokea rushwa ya Sh 73,000.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa, Mpalaza ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Ardhi katika Kata ya Nsalala alidai rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ahadi Ndile kwa lengo la kumpatia hukumu iliyotolewa na Baraza hilo.

Ndile alikuwa kwenye mzozo wa mpaka na Diwani wa Kata ya Ikukwa Viti Maalumu, Monica Degua (CCM) na Baraza hilo lililopo Mbeya vijijini lilimpa ushindi Degua. Ndile alithibitisha kutokea tukio hilo akisema;

“Sikuridhishwa na hukumu ya Baraza, nikaamua kuomba nakala ya hukumu ili nisonge mbele, mwanzo waliniambia nipeleke Sh 10,000 ili niandikiwe taarifa nzuri sana.

“Nilipokwenda na fedha hizo ambazo walidai ni gharama za Baraza, walidai hazitoshi na nitapewa endapo tu nitapeleka Sh 73,000. Sikuona sababu ya kupeleka fedha hizo ndipo nilipowasiliana na Takukuru ambao leo (jana) wamefanya kazi yao,” alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya, Daniel Mtuka alikiri kumshikilia Mpalaza kwa tuhuma hizo kwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Asia Haruna.

Akizungumzia tukio hilo alisema Novemba 26 mwaka huu ofisi za Takukuru mkoani hapo zilipata taarifa kutoka kwa mlalamikaji aliyefahamika kwa jina la Ahadi Ndile ambaye alikuwa na kesi ya madai namba 26, 2012 ya kugombea mpaka yeye na jirani yake Monica Degula.

Alisema kutokana na mgogoro huo wa mpaka, walipeleka kesi katika Baraza hilo ambapo baada ya uamuzi, Ndile alishindwa na Monica na hakuridhika na uamuzi huo na hivyo kuamua kuomba kupatiwa mwenendo wa shauri pamoja na hukumu.

Mtuka alisema wakati akiomba kupatiwa hukumu hiyo ndipo alipotakiwa kuhonga Sh 73,000 kwa Mpalaza ambaye ni Katibu wa Baraza hilo ikiwa ni pamoja na Sh 10,000 kwa ajili ya gharama ya kesi.

Hata hivyo Mtuka alisema migogoro ya ardhi imekuwa kero katika eneo hilo na kwamba Takukuru ina majalada mengi yatokanayo na malalamiko kutoka kwa wananchi wakitakiwa kutoa rushwa na kudhulumiwa haki zao.

Alisema bado wanahojiana na Ndile pamoja na Mwenyekiti lakini aliyepokea fedha hizo ni Mpalaza.
hii kweli kali, yaani ma prochadema mnatetea mpaka rushwa kisa ni kiongozi wa chama? whats hell is this?
 
kama kweli anahusika achukuliiwe hatua za kisheria,illa sio kuchufuana kisiasa.!!
 
Imeandikwa tarehe 05 Desemba 2012 | Mwandishi wa HabariLeo

........alidai rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ahadi Ndile

Hivi huyo jamaa alikuwa anategemea nini kama si kudhalilishwa! Jana ulikuwa majukwaani unautangazia ulimwengu kwamba CCM wanakula rushwa leo unashuka na kwenda kuwaomba rushwa! Akili kweli ni nywele na kila mtu ana zake.
 
Hivi huyo jamaa alikuwa anategemea nini kama si kudhalilishwa! Jana ulikuwa majukwaani unautangazia ulimwengu kwamba CCM wanakula rushwa leo unashuka na kwenda kuwaomba rushwa! Akili kweli ni nywele na kila mtu ana zake.

Umecomment vizuri sana ,unajua hakuna binadamu aliyekamilika kwa asilimia 100,lakini cha ajabu kuna watu humu Jamvini wanachangia utadhani walioko CDM wote ni wasafi na watakatifu!!!!!!jamani mwogopeni mungu tunakoelekea sio kuzuri.
 
hicho chanzo cha habari kinaifanya habari yote iwe takataka...mnajitahidi sana lakini tutawang'oa tu madarakani.

Chadema ni watanzania kama wewe na pia wana kasoro nyingi tu. Hivi kwa nini unadhani wao ni malaika? Tumia talanta aliyekupa Mungu kufikiria na si kubeza kila kitu. Hivi watu kama nyinyi ndio mpewe uongozi hata wa mtaa mnafaa kweli?. Akili finyu, uwezo wa kufikiri mdogo, uwezo wa kujua mambo haupo. Bahati mbaya gani hii? Kuna kazi kwelikweli
 
Cdm wanajifanya wasafi sana kama mohamed morsi na muongo ukweli hujidhihirisha.cdm ni wala rushwa wakubwa maka ya ngono.
 
Chadema ni watanzania kama wewe na pia wana kasoro nyingi tu. Hivi kwa nini unadhani wao ni malaika? Tumia talanta aliyekupa Mungu kufikiria na si kubeza kila kitu. Hivi watu kama nyinyi ndio mpewe uongozi hata wa mtaa mnafaa kweli?. Akili finyu, uwezo wa kufikiri mdogo, uwezo wa kujua mambo haupo. Bahati mbaya gani hii? Kuna kazi kwelikweli
nani alikwambia nataka uongozi?hata kama unaniambia uelewa wangu finyu lakini nina uwezo wa kujua kuwa dr dr dr dr dr dr jakaya kikwete alihongwa suti tano na waarabu akawapa kilimanjaro hotel
kikwete ndiye mwenye richmond/dowans(swahiba wake lowassa alithibitisha pasi shaka
meli ya katibu mkuu wa ccm(kinana)ilibeba pembe za tembo zilizoibiwa kwenye mbuga zetu
kikwete aliingia madarakani kwa hela ya wizi(kagoda)
kikwete aliwaita wezi wa epa na kuwasamehe na kuwapa chai ikulu
aliyemteka ulimboka ni afisa wa ikulu.......
nk nk nk nk
koma kuvamia jamvi la weledi
 
Imeandikwa tarehe 05 Desemba 2012 | Mwandishi wa HabariLeo

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) James Mpalaza wa Wilaya ya Mbeya Vijijini amenaswa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) akipokea rushwa ya Sh 73,000...

Yani hiyo ndio habari, nafikiri habari za aina hii zitakuwa zinatafutwa sana na CHADEMA wajiangalie maana hakuna nafasi ya kufanya makosa watu wanawatolea macho.
Kikubwa zaidi ni wanachama na viongozi waelewa kinachohubiriwa na chama na waamini katika hayo kwa kuyafuata kivitendo
 
Kumbe gazeti lenyewe Habari Leo hapo hakuna kitu ni uhuni tuu wa gazeti,tuleteeni fedha zetu mlizokwiba na kuzipeleka Uswisi,mwambieni Kina..na arudishe wanyama wetu ambao hizo fedha ndizo wanazotumia kuhonga wapinzani.

Hata mimi baada ya kuona hiyo Source tu imani imenitoka na kuona habari yenyewe ni Takataka.
 
Njaa mbaya katibu wa Chadema Mbeya 73,000 imemtoa imani.
Yaa bora hawa walioficha uswis wa CCM ambao dola inawalinda, wameficha nyingi njaa hawana, ingawa wanaua watu mahospitalini na kufelisha wanafunzi mashuleni
 
Hata mimi baada ya kuona hiyo Source tu imani imenitoka na kuona habari yenyewe ni Takataka.

Mkuu ni vyema kuujua ukweli ili habari ikanushwe au inyooshwe kuliko kuiona tu takataka, huwezi jua wengine wataionaje
 
Imeandikwa tarehe 05 Desemba 2012 | Mwandishi wa HabariLeoTaarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa, Mpalaza ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Ardhi katika Kata ya Nsalala alidai rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ahadi Ndile kwa lengo la kumpatia hukumu iliyotolewa na Baraza hilo.
Hapa ndio uongo ulipo, hata kama huna akili na una njaa kiasi gani huwezi kwenda kuomba rushwa kwa CCM.
 
Back
Top Bottom