DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi anatuhumiwa kuhusika katika mipango ya kuiba kura za maoni kuelekea uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2025, ili kumuwezesha Mbunge aliyepo madarakani, Jimbo la Mufindi Kusini Mhe. Davidi Kihenzile, kuendelea kushikilia nafasi hiyo kupitia tiketi ya CCM.
Tuhuma hizo zimetolewa hadharani na kada wa chama hicho, Salimu
“Huu ni mpango mchafu wa kupindua demokrasia ndani ya chama, Tunaitaka Kamati Kuu ya CCM kuingilia kati, uchaguzi usogezwe mbele ili kupisha uchunguzi huru,” alisema Nyomolelo mbele ya wanahabari.
Aidha, Nyomolelo alieleza kuwa kuna taarifa za ndani zinazoonyesha kuwa kila kura ya uungwaji mkono inalipiwa shilingi 50,000 kama sehemu ya kuhakikishwa Mbunge huyo anapita bila ushindani wa haki.
Hata hivyo Nuru digital imemtafuta Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi na kukataa kuwa hana taarifa hizo na kuelekeza atafutwe katibu ndiye mwenye taarifa hizo.
Nuru Digital imefanikiwa kumpata Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Clemence Bakuli ambaye alikanusha vikali tuhuma hizo, akizitaja kuwa ni uzushi usio na msingi wowote
Akizungumza kwa njia ya simu “Huo ni uzushi mtupu. Taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa kwa mujibu wa kanuni na hakuna mpango wa namna hiyo unaofanyika ndani ya chama,” alisema Katibu huyo kwa njia ya simu.
Hata hivyo vuguvugu la malalamiko kutoka kwa wanachama na wadau wa siasa wilayani Mufindi linaendelea kushika kasi, wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kurejesha imani ya wanachama kwenye mchakato wa kidemokrasia ndani ya chama hicho tawala.
Tuhuma hizo zimetolewa hadharani na kada wa chama hicho, Salimu
, aliyedai mbele ya vyombo vya habari kuwa njama hizo zinashirikisha pia Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi, huku baadhi ya wajumbe halali wa mkutano wa uchaguzi wakiondolewa kwa makusudi na wengine "feki" kuingizwa kwa hilo“Huu ni mpango mchafu wa kupindua demokrasia ndani ya chama, Tunaitaka Kamati Kuu ya CCM kuingilia kati, uchaguzi usogezwe mbele ili kupisha uchunguzi huru,” alisema Nyomolelo mbele ya wanahabari.