Katibu wa CCM mbaroni kwa uchochezi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mpanda, Jacob Nkomola, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi na kuhamasisha vijana kuandamana hadi nyumbani kwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, Padri Patrick Kasomo ili wamvue joho la kichungaji na kumpiga, kwa kuwa hana sifa za kuwa kiongozi wao wa kiroho.

HabariLeo.
 
Ahaa, huu si ndo anaohubr raisi?. Thank God kuwa watu wake wanatekeleza ajenda yao! Kumpiga kiongozi wa dini? Hajui nguv ya Mungu
 
Hivi ktk ccm kuna nin? Mbona wanajichukulia hatua pasipo kujua sheria za nchi? Na yule Mgombea Ubunge wa Maswa Magharibi, aliyempiga ngwara OCD yupo wap? Alichukuliwa Hatua zipi?
 
Ahaa, huu si ndo anaohubr raisi?. Thank God kuwa watu wake wanatekeleza ajenda yao! Kumpiga kiongozi wa dini? Hajui nguv ya Mungu
Wanatekeleza maagizo ya Mwenyekiti wao kupiga viongozi wote wa dini.
 
Hahaaaa CCM bwana...wasione kichaka.............
 
hii! ni kiini macho, wana taka kuhalalisha watakapowageukia cdm, tena uongozi wa juu
 
hii! ni kiini macho, wana taka kuhalalisha watakapowageukia cdm, tena uongozi wa juu

Hapo umenena mwanagu. Nadhani ni muda muafaka kwa viongozi wa ngazi zote wa CDM kujiepusha na lolote lihusulo uchochezi. Maana hawa jamaa wameanza kumtafuta mchawi mwituni. Plse! take care!!!
 
Huyo ni mmoja wa vijana katika kikosi kazi cha mheshimiwa Pinda katika propaganda na mipango yote ya kichama huko Mpanda,nadhani katumwa kufanya hivyo maana sidhani kama kwa utashi wake anaweza kuchochea jambo kama hilo.
 
Hakuna askofu mwenye jina hili Tanzania. Askofu wa Mpanda anaitwa WILLIAM, Paschal Kikoti.
 
jamani naomba mnisaidie wakatoliki, hivi kuna jimbo la mpanda kweli? Mie najua jimbo ni sumbawanga (wala sio rukwa wala mpanda) ambalo linapakana na jimbo la kigoma, tabora na mbeya. Mtuma post hujakosea kama habari leo wameandika hivyo, wao habari leo ndio watakuwa wameupotosha umma kuhusu ukweli wa jimbo husika. Naomba kutoa hoja
 
Walioko huko watusaidie.Ila nahisi alitaka kusema "Paroko" na wala siyo Askofu.
 
Huyu ni naibu askofu (Vicar), juzi alizuia makanisa kadhaa jimboni kwake kupokea msaada uliotolewa na mbunge wa CCM huko baada ya kukashifiwa na huyo Nkomola. Nadhani hii ya kususia misaada ndiyo imeishtua serikali. Kama sijasahau, huyu Nkomola amewahi kuwa kiongozi CHADEMA.
 
Hakuna askofu mwenye jina hili Tanzania. Askofu wa Mpanda anaitwa WILLIAM, Paschal Kikoti.

jamani naomba mnisaidie wakatoliki, hivi kuna jimbo la mpanda kweli? Mie najua jimbo ni sumbawanga (wala sio rukwa wala mpanda) ambalo linapakana na jimbo la kigoma, tabora na mbeya. Mtuma post hujakosea kama habari leo wameandika hivyo, wao habari leo ndio watakuwa wameupotosha umma kuhusu ukweli wa jimbo husika. Naomba kutoa hoja
HabariLeo

Katibu wa CCM mbaroni
Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 5th March 2011 @ 09:50 Imesomwa na watu: 268; Jumla ya maoni: 0


JESHI la Polisi wilayani Mpanda limemkamata Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo, Jacob Nkomola, kwa tuhuma za kumtolea maneno ya kashfa na kumtishia maisha Makamu wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, Padri Patrick Kasomo.

Kukamatwa na kuhojiwa kwa Katibu huyo wa CCM kunatokana na kufunguliwa kwa jalada namba RB/849/2011 na Padri Kasomo dhidi yake juzi kwenye Kituo Kikuu cha Polisi mjini humo.

Kasisi huyo ambaye pia ni Paroko wa Kanisa Katoliki Karema anadai Nkomola alitoa pia maneno ya uchochezi akihamasisha vijana kuandamana hadi nyumbani kwake (Kasomo) ili wamvue joho la kichungaji na kumpiga, kwa kuwa hana sifa za kuwa kiongozi wao wa kiroho.
Inadaiwa maneno hayo ya kejeli na kashfa pamoja na kutishia maisha aliyatoa alipohutubia mikutano kwenye vijiji vya Karema na Kaparamsenga, iliyoitishwa na Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso kwa lengo la kushukuru wananchi kwa kumchagua.

Hadi jana haikuwa imefahamika mara moja kama Katibu huyo ataachiwa kwa dhamana au la, kwani ilielezwa kuwa bado anaendelea kutoa maelezo kwa maandishi kituoni hapo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaluanda, alithibitisha kukamatwa na kuhojiwa kwa Katibu huyo, na kuongeza kuwa kasisi huyo aliamua kumshtaki baada ya jitihada za usuluhishi za Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo kushindikana.

Mwaluanda alisema mgogoro baina ya wananchi na Kanisa, unatokana na kumtuhumu Kasisi huyo kuwa amepora sehemu kubwa ya ardhi kijijini humo yakiwamo maeneo ya wazi; moja likiwa ni uwanja wa kuchezea mpira ambao alipitisha trekta na kuubadili kwa ajili ya shughuli za kilimo ambapo limepandwa miti .

Hata hivyo habari ndani ya Jeshi la Polisi Mpanda zinadai kuwa upo uwezekano mkubwa Katibu huyo wa CCM kufikishwa mahakamani kesho kutwa.
 
Kama Padre amepora ardhi kwanini naye asishitakiwe? Isijekuwa maeneo hayo ya wazi yalikuwa ya Kanisa na wanakijiji kwa mazoea ya kuyatumia siku nyingi kwa michezo wakafikiri ni ardhi ya kijiji!
 
Wanaandaa mazingira ya kukamata viongozi wa Chadema. Changa la macho hilo.
 
Its obvrous kama padri huyo kapora ardhi ya wananchi sheria itachukua mkondo wake lakini kitendo cha huyo kiongozi wa ccm kutamka maneno hayo hakikubaliki huu ndio uchochezi wa wazi kuwahamasisha watu waandamane mpaka kwa padre wakamvue joho na kumpiga. Nategemea viongozi wa kitaifa wa ccm taifa watoe matamko ya kulahani kauli hizo za kiongozi wao wa mpanda sio kukaa wanalaani maandamano ya amani ya chadema.
 
juzi tu hapa kanisa katoliki wilayani mpanda lilikataa msaada wa mbunge wa ccm leo mnadai kuwa askofu amepora ardhi? kwani katibu wa ccm ndiye afisa ardhi au afisa mipango miji wa mpanda hadi atoe maelezo juu ya umiliki wa ardhi? me naona ni njia ya kuonyesha hasira yao ya kukatatliwa kwa msaada wao na kulichafua kanisa.
 
Back
Top Bottom