Katibu wa CCM Kata ya Mtindiro ajiunga CHADEMA

Katibu wa CCM Kata ya Mtindiro ajiunga CHADEMA

Kicheba One

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
399
Reaction score
194
Katibu huyo ndugu hatibu manga ameamua kujiunga na chadema baada ya kugundua kuwa amepotea njia,pia katibu huyo amesema wananchi wa kata ya mtindiro wana onewa sana kwa kukosa bara bara nzuri,ushuru wa machungwa na mahindi kwa wakulima ambao sio wafanya biashara,michango ya mwenge,michangoya maabara na misaragambo isiyo na mipaka huku ruzuku za vijiji zikitafunwa ovyo,hivyo kada huyo amejiunga chadema kuongeza nguvu za mapambano ya kukombozi muheza;katibu wa chadema muheza lukindo mohamed amempokea kwa kumkabidhi kadi ya chadema
 
Futeni kabisa ccm hapo muhenza tanga
 
Naomba tafsiri ya misaragambo mkuu .
Misaragambo ni kazi zinazofanywa na wananchi kwenye vijiji/vitongoji kama vile kuchimba barabara, kutengeneza matofali kwa ajili ya shule/zahanti/ huko kwenu mnaita Nguvu za wananchi! Kisheria msaragambo unapangwa na Mkutano mkuu wa Kijiji na unakuwa ni sehemu ya sheria ndogo ndogo za vijiji (by laws) na unatakiwa ufanyike mara moja kwa kwa siku za wiki! Msaragambo haupangwi na Halmashauri ya kijiji au mwenyekiti na Mtendaji wake bali ni azimio linakuwa limetolewa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa Kijiji!
 
karibu kwenye ukombozi kuweni makini usikute ccm wamemtuma kuja kutuvuruga
 
Kama ambavyo chadema ni chama kilichoonyesha kuwakomboa watanzania waliopigika, walioteswa na kukatishwa tamaa na ccm, watu ambao wamejitambua kuwa ccm ni janga la taifa, tunamkaribisha chadema.

Hongera kwa kujitambua
 
ccm inazidi kusambaratika kila ck chdm wanavuna kushoto na kulia wallahi hadi dec atabaki ki...., na.....pe na mgulo.

Ila habari ya kushangaza tanga kuna mdudu anaitwa msaragambo ambapo kila jmos 1 ktk wiki maduka yote ndani ya jiji (CITY) hufungwa kuanzia alfajiri hadi sa 4. Usiombe siku hiyo ushikwe na tumbo la kuhara au maradhi yoyote yatakayokulazimu kutafuta dawa kwenye maduka ya dawa ITAKULA KWAKO, maduka yote katikati ya jiji yanafungwa halafu bado hili eti ni jiji hao wafanyakazi wa halmashauri wanaopaswa kukagua usafi wako wapi?

Huwa nahoji ubunifu wa viongozi wa ccm ukoje ksbb zipo alternatives nyingi za kuwafanya wananchi wafanye usafi na si kuwalazimisha wafanyabiashara kufunga maduka. Hebu piga picha maduka yote dar yafungwe kwa masaa ma4 eti watu wafanye usafi............................
 
mpaka wachanganyikiwe mwaka huu chadema shikilia hapohapo
 
Hahahaha muheza wamejitambua sasa......ccm itabaki kwny magazeti ya Uhuru tuu
 
Back
Top Bottom