Mwanagandila
Senior Member
- Oct 9, 2011
- 182
- 100
Baada ya kutangaza kuvunja mkataba klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima, Katibu wa klabu hiyo Dr Jonas Tiboroha sasa amekalia kuti kavu kutokana na kufanya maamuzi ya kukurupuka.
Taarifa za ndani ya klabu hiyo yenye makao yake mitaa ya twiga na jangwani zimesema, uongozi huo tayari unapanga kuachana na Tiboroha ifikapo Ijumaa mosi 2016 mwaka mpya, na nafasi hiyo kuchukuliwa na meneja Masoko wa TFF Peter Saimon.
Hivi karibuni Tiboroha aliwagawa wanachama wa klabu ya Yanga, kufuatia kuvunja mkataba na Haruna Niyonzima, huku pia akimtaka mchezaji huyo kuilipa klabu hiyo U$ 71,000 sawa na milioni 149 za kitanzania.
Sababu zilizotolewa kupelekea kuvunja mkataba huo ni kushiriki michuano isiyotambulika ya CECAFA, jambo ambalo wadau wa soka limewashangaza kwani michuano hiyo inatambulika CAF na FIFA, Tanzania ikiwa mwanachama wa michuano hiyo, iliyopelekea kusimamishwa kwa Ligi Kuu ya Vodacom kutoa nafasi kwa timu ya Kilimanjaro Stars kushiriki michuano hiyo.
Kujiunga na timu ya Taifa ya Rwanda AMAVUBI bila mwaliko, taarifa zinaonyesha Haruna Niyonzima ana barua za mwaliko kwa kila kalenda ya FIFA kutoka FERAFWA nchini Rwanda kumuomba mchezaji huyo kuitumikia timu yake ya Taifa na mialiko hiyo hutumwa moja kwa moja TFF na nakala zake kwenda katika klabu ya Yanga.
Kuchelewa kurudi anapokua Rwanda, mchezaji Niyonzima amewahi kupewa onyo kwa mdomo mara moja tu bila maandishi yoyote, kitu ambacho kisheria hakina ushahidi.
Kufuatia sababu hizo zilizotolewa na Yanga kupelekea kuvunja mkataba dhidi ya Niyonzima, zimeonekana kutokua mashiko kwani katika mkataba wake hakuna kipengele kinachoelezea juu ya kuvunja mkataba endapo mchezaji atachelewa kurudi/kuripoti kwenye kituo chake cha kazi.
Mpaka sasa Yanga haijamkabidhi Niyonzima barua ya kuachana nae ikiwa ni siku ya tatu tangu kutangaza kuachana nae kwa kukiuka mkataba.
Pamoja na Yanga kutangaza kumdai Niyonzima zaidi ya mil 149, Sheria za FIFA hazimzui mchezaji kusajiliwa au kucheza klabu nyingine wakati shauri lake likiwa linasikilizwa.
Yanga itamkosa Niyonzima, lakini pia itapaswa kumlipa mchezaji huyo kwani yenyewe ndio itakua imevunja mkataba, na mchezaji huyo atakua huru kuchezea klabu yoyote duniani itakayo msajli katika kipindi hiki cha dirsha dogo la wakati wa baridi.
Baada ya kupitia vifungu vya CAF na FIFA juu ya uvunjwaji wake mkataba huo, uongozi wa Yanga umeona katibu mkuu huyo amekurupuka bila kujua sheria zinazoongoza soka duniani zinaelekeza nini, na kuifanya klabu hiyo sasa kuwaza njia ya kumlipa mnyarwanda huyo pesa zake kwa kuvunja mkataba.

Last edited: