GE2025 Katibu Mkuu wa Chama MAKINI: Tutapeleka waandishi Canada, Wazee Posho laki 1 kila mwezi na Vijana kupewa bodaboda bure

GE2025 Katibu Mkuu wa Chama MAKINI: Tutapeleka waandishi Canada, Wazee Posho laki 1 kila mwezi na Vijana kupewa bodaboda bure

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Katibu Mkuu wa Chama cha Maarifa, Kilimo na Nishati (Makini), Ameir Hassan Ameir, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho uliofanyika Septemba 2, 2025, katika eneo la Manzese jijini Dar es Salaam, amesema endapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza dola, kitaweka mpango maalumu wa kuboresha utendaji wa wanahabari kwa kuwapeleka nchini Canada kupata semina za kuongeza ujuzi ili wafanye kazi kwa weledi zaidi.

Pia amesema Chama cha Makini kitaanzisha mfuko (Makini Fund) ambapo kina mama wote watapewa mikopo bila masharti, ukipewa laki moja unarudisha laki moja, ukipewa milioni moja unarudisha milioni moja,e, na vijana kupewa bodaboda bure ambapo kwa awamu ya kwanza watatoa bodaboda Millioni 1 bure na Wazee kupewa Laki moja kila mwezi.


 
Back
Top Bottom