Ndani ya chadema kila mtu ni kambale. By Duni Haji.
Maana ya kauli hii ni kwamba "ndani ya chadema hakuna nidhamu".
Aliyasema maneno hayo babu Duni alipokuwa akirejea rasmi ktk chama chake baada ya kuwa ndani ya CHADEMA kwa miezi kadhaa. Ni dhahiri aliyaona mengi ndiyo maana akahitimisha kwa kauli hiyo ambayo hadi leo haijatolewa tamko lolote na viongozi wa ngazi ya juu ya CHADEMA.
Naandika uzi huu baada ya kuona uzi humu ndani unaoeleza kuwa mbunge viti maalumu (CHADEMA), Mhe. Ruth Mollel analaumu maamuzi na msimamo wa chama chake kutohudhuria vikao vinavyoongozwa na NS. Huu ni ukambale.
Mbona CUF wametupa pesa zao ktk uchaguzi wa 2015 na ulipofutwa wakasusa kushiriki ule wa marudio. Wametoa sadaka nafasi zao za uwakilishi (ubunge) kwa maslahi mapana ya ustawi wa demokrasia Zanzibar. Hatujamsikia si mwakilishi ama diwani akitoa kauli kama za Ruth Mollel. Ni kweli ndani ya CHADEMA kuna ukambale.
Kwa hili katibu mkuu fungua mlango wa ofisi yako toka nje ulikemee. Vinginevyo ukambale huu utaharibu si tu msimamo wa chama chako juu ya NS, bali pia taswira ya chama chako miongoni mwa jamii.
Chama lazima kiwe na msimamo hata kama kimekosea lazima muulinde msimamo wenu. Vinginevyo mtaonekana wakurupukaji.