Wanakusanya kwa niaba ya halmashauri. Lazima mkataba uheshimiwe!Kwani hao wafanyibiashara wanakusanya hayo mapato kwa niaba ya halimashauri?Kama sio Katibu haoni kwamba anaikosesha halimashauri mapato?Na hata kama hao wafanyibiashara wanakusanya mapato kwa niaba ya serikali labda DC kaona kuna ujuaji.Dah,pole zake Humphrey,siasa ni ngumu sana.Kiutendaji hii inakatisha tamaa sana.Humprey aachie ngazi tu,hatawezana na waswahili hao.
watu wanajenga nyumba moja lakini wanagombania fito.Why Comrade?
Mzee Tupatupa
Uko sahihi sana Mkuu. Kampuni ya Majimoto,ya wafanyabiashara haohao,ina mkataba wa pango na mmiliki halali wa eneo ambaye ni Kiwanda cha Urafiki. DC Polepole ametumia ubabe tu kutwaa eneo hilo. Amewamwagia majigambo na nyodo nyingi wafanyabiashara hao.Wanakusanya kwa niaba ya halmashauri. Lazima mkataba uheshimiwe!
Wanakusanya kwa niaba ya halmashauri. Lazima mkataba uheshimiwe!
Hivi ni tangu lini dc akawa mkusanya mapato ya serikali?hii nchi ni zaidi ya tuijuwavyoKatibu Mkuu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa,Mhandisi Mussa Iyombe amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole kuacha utaratibu wa wafanyabiashara wa Soko la Ndizi Mabibo uendelee.
Katibu Mkuu Iyombe ametoa agizo hilo jioni ya leo alipokutana na wawakilishi wa wafanyabiashara wa soko hilo ofisini kwake. Akitoa agizo hilo kupitia kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo,Katibu Mkuu Iyombe ametaka utaratibu wa kukusanya ushuru na ulipaji kodi uliokuwepo uendelee.
Katibu Mkuu Iyombe amesema kuwa kama kutakuwa na haja ya mabadiliko au maboresho yoyote,wafanyabiashara wahusishwe. DC Polepole 'alilichukua kimabavu' soko la Mabibo na kuanza kukusanya mapato sokoni hapo kupitia watumishi wa Halmashauri bila kujali uwepo wa Kampuni ya Majimoto ya wafanyabiashara hao iliyopangishwa eneo hilo na Kiwanda cha Urafiki,mmiliki wa eneo husika.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kwani jechaa si atakuwepo?Wakivurunda si wanapangiwaga kazi nyingine, acha wafanye kazi kwa mizuka na makeke.
2020 tutawahakiki.
Naona unamtafuta cha moyoni polepole,unataka watoto wake wakose ada?Ndio maana Hamphrey Polepole alitoa maoni mazuri sana katika makongamano ya Rasimu ya Warioba kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana kazi. Hivi vyeo vifute. Kwa nini Raisi wetu mpendwa hataki kufuata ushauri wa HampreyPolepole?
Ccm wamezidi kwa maigizoNgojeni uchaguzi mdogo wa madiwani upite muone watakavyowageuka.
Ccm wanachohitaji ni kuwalaghai wananchi ili wapate kura tuNchi hii imekuwa kama shule kila mwalimu anafundisha somo lake kwa wanafunzi wale wale na lengo ni moja tu kufaulisha mitihani na sio kumjenga mwanafunzi kuelewa somo husika
Ogopa sana njaaNaona Baada ya Hili Karipio,Polepole Atatoka Hadharani na Kuliunga Mkono Tamko Hilo kwa Kukiri Kuwa Vyeo vya uDC na uRC,Havina Tija!Kama Yeye Alivyooneshwa Leo!
na hivi wamekaa mkao wa kuchimbana na kutafutana na yule mpenda kiki aliyempiga makofi warioba.Polepole amepata pigo la Mwenyezzi Mungu kwa usaliti wake amekaa na mkuu wa mkoa anayemuogopa asije akapewa yeye ukuu wa mkoa kwa sababu kichwani mwake hana mipango sasa wanamkandamiza amebaki kulalama facebook wanajifaanya hawaoni hilo ndilo tunda la kusaliti wananchi na kutukana watu wazima bado kufa tu kwa sasa ni very irrelevant hawezi hata sema kitu channel ten watu wakamsikiliza
Tatizo hii sanaa ya "utumbuzi" mumeibeba vibaya, mkataba kama una tatizo au kama wenyewe mnavyoita dili, kuna taratibu za kushughulikia! Zifuatane tu hizo taratibu!Hapo ndipo penye shida.Mikataba yote iliyoingiwa kwenye awamu ya nne ni utata mtupu.Kwa sababu hiyo kwa maslahi ya nchi hasa ukizingatia kwamba kilichokuwa kinaendelea ni ulaji mtupu, ni lazima mkataba huo uvunjwe.Kwa taswira hii napata picha kwamba Katibu Mkuu Tamisemi naye ana maslahi katika dili hilo.Atumbuliwe tu.