GE2025 Katibu Mkuu, TAHLISO: Malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uongozi na Katiba dhidi ya Rais Geofrey Kiliba kwa upendeleo wa Kisiasa

GE2025 Katibu Mkuu, TAHLISO: Malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uongozi na Katiba dhidi ya Rais Geofrey Kiliba kwa upendeleo wa Kisiasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mimi, Dickison Damasi, mwanachuo katika moja ya Vyuo vilivyopo Dar es Salaam na mwanachama hai wa TAHLISO, napenda kuwasilisha malalamiko rasmi dhidi ya Rais wa sasa wa TAHLISO, ndugu Geofrey Kiliba, kutokana na madai ya kuhusika moja kwa moja na shughuli za chama fulani cha siasa kinyume na katiba, maadili na misingi ya taasisi yetu.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 4(a) cha Katiba ya TAHLISO, taasisi hii ni "non-partisan", isiyofuata vyama vya siasa katika shughuli zake.

Aidha, Kifungu cha 76-Leadership qualities kinasisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuwa waadilifu, wasiochochea itikadi, na kutekeleza utekelezaji wao kwa uwazi na usawa.

Kwa masikitiko makubwa raisi wa tahasisi hii ambaye ana wajibu wa kuwasemea wanafunzi na changamoto zao amekua msemaji wa ccm. Hivyo kuwabagua hata wale anawaongoza ambao hawafungamani na upande wowote wa vyama vya siasa.

Kwa kuzitaka tahadhari na uwazi kwenye utekelezaji, ninatoa malalamiko haya rasmi na ombi lifuatalo:

1. Uchunguzi wa haraka, wa huru na wa haki ufanyike ili kubaini ukweli kuhusu madai hayo.
2. Hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo kusimamishwa kwa muda, au kivuliwa madaraka, kama madai yatathibitishwa.
3. Matokeo ya uchunguzi yafahamishwe kwa umma wa wanachama wa TAHLISO, ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji.

Katika uchunguzi pia endapo itahitajika msaada wa recorded clips zipo na ntakua tayari kuzitoa kudhibitisha madai haya.

Mwisho napenda kuwafahamisha viongozi wote wa TAHLISO kupitia ofisi yako wanaoendelea kuvunja katiba yetu na kuwaomba kwa mara ya mwisho kwa upendo na kuacha kujihusisha na siasa kupitia taasisi yetu.

Endapo hali hii ikiendelea basi hatua zaidi zitafuata ikiwa ni Pamoja na kufungua kesi mahakamani kwa taasisi kama watu binafsi tunaomba msimamie maslahi ya wanafunzi tu.

Nina imani kuwa ofisi yako itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa kanuni za uongozi bora, usawa, uwajibikaji na heshima kwa katiba ya wanafunzi. Pia naomba utekelezaji na majibu ya barua hii yajibiwe kwa mfumo rasmi wa barua.


1753705171168.png

1753705191040.png
 
Kumbe wapo wana TAHLISO ambao UPSTAIRS wapo vyedi.. maana huyo " Rais" wao huwa simuelewi na sodhani hata kama ameshawahi kuisoma Katiba ya TAHLISo na ToR yake
 
Back
Top Bottom