Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,314
- 72,740
Chama cha Mapinduzi kilikuwa kimejipanga vyema kabisa na lundo la tuhuma na kashfa mbalimbali kwa watu kadhaa ambao walikuwa katika list yao kuwa watakuwa wateule wa Ukatibu mkuu wa Chadema.
Habari za uhakika zilizopatikana toka ndani ni kuwa kitengo cha propaganda cha ccm kwa muda wa miezi minne kilipewa jukumu la kufanya kazi hiyo ya kutafiti kasoro za mmoja mmoja kwa wale watu sita ambao wao walisema panga pangua lazima awe mmoja wao.
Kasoro na kashfa hizo zilikwishaandaliwa makala kila mtu na yake ikitegemea nani atatangazwa. Project hii iligharimu fedha nyingi zilizotengwa na chama.
Lakini kitendo cha Chadema kuja na jina geni kabisa kwao ni sawa na kupigwa knock out dakika ya kwanza ya round ya kwanza. Hawakutegenea na wamepigwa butwaa.
Wapo viongozi ambao walikuwa na kikao cha siri hotelini maeneo ya Mikocheni wakisubiri jina litajwe walionekana wakitawanyika usiku wakiwa wameinamisha vichwa chini.
Hata kwenye mitandao ya jamii ambako watu walikesha wakisubiri wachangiaji wengi waliokuwa wanasubiri kuiponda Chadema kwa yale majina waliyokuwa nayo wamechanganyikiwa na kumshambulia Dr Vicent bila mpangilio maana hawamjui.
Chadema kumbe inajua kucheza na siasa za CCM kwa nini haikamati dola kwa mbinu hizi? Hilo ni swali katika mada nyingine