Katibu Mkuu, Kinana na timu yake watua katika Jimbo la Mwigulu Nchemba, ahutubia umati wa watu.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264

Sehemu ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiwa na Naibu Katibu Mkuu Mh. Mwigulu Nchemba katika maandalizi ya kumpokea Katibu Mkuu.

Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara akimpokea Katibu Mkuu CCM-Taifa Mh. Kinana alipowasili Jimboni Iramba kwa ajili ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Wilaya ya Iramba.


Katibu Mkuu akikaribishwa na wananchi kwa ngoma za asili.

Mwigulu Nchemba akicheza ngoma ya asili.




Katibu Mkuu CCM Taifa Mh. Kinana akishiriki na wananchi katika Ujenzi kwenye Kituo cha Afya cha Kaselya Jimboni Iramba


Katibu Mkuu Kanali Mstaafu Kinana akipanda Mti wa Kumbukumbu kwenye Kiwanda cha Kuchuja Alizeti Kata ya Ndago.

Hili ni jengo la Kituo cha Afya kata ya Shelui ambalo linajengwa kwa Nguvu za Wananchi wakisaidiana na Mbunge wao, Mh. Mwigulu NChemba.

Katibu Mkuu akijumuika katika ujenzi wa jengo hilo.

Mh. Mwigulu Nchemba akiweka sawa Zege kwenye Ujenzi wa Kituo cha Afya Shelui ambacho amechangia Mifuko 100 ya sementi kwenye Ujenzi wa Kituo hiki.




Katibu Mkuu akiwasili viwanja vya stendi Kiomboi katika mkutano wa hadhara.




Sehemu ya umati wa Wananchi wakionesha hisia zao za furaha mara baada ya Msafara wa Katibu Mkuu kuwasili Kwenye eneo la Mkutano-Kiomboi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Moses Nnauye akiwahutubia Wananchi wa Iramba-Kiomboi, Kubwa amesisitiza WanaCCM kuwa Wamoja kwasababu kuna baadhi ya Vyama vya Upinzani vinajenga mafarakano katika Taifa kwa malipo ya madaraka. Viongozi hawa wanadiriki mpaka kutoa matusi na dharau kwa waasisi wa Taifa letu ambao wamelijenga taifa linalowawezesha kupata nafasi ya kuingia kwenye bunge na kuanza kutukana na kukejeli juhudi za Wazee wetu.


Mwigulu akiongea na wananchi wapiga kura wake kuhusu mafanikio na mikakati katika utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo lake.

Mwigulu Nchemba na Nape Nnauye wakiwa kwa pamoja jukwaani.

Katibu Mkuu akiwa jukwaani na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mzee Msindai.

Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dkt. Parseko. V. Kone
 
Mheshimiwa Mwenyekiti
Rasimu ya Katiba ni kitabu kikubwa kilichosheheni mambo mengi. Kina kurasa 106, sura 17 na ibara 271. Wajumbe wa Bunge hili mnatakiwa kusoma na kuelewa vizuri kila kilichoandikwa ili muweze kufanya uamuzi ulio sahihi. Mnawajibika kuchambua kwa kina na umakini mkubwa kila kilichomo, sura kwa sura, ibara kwa ibara, sentensi kwa sentensi na hata neno kwa neno. Hamna budi kujiridhisha kuhusu uandishi wa vifungu vya Rasimu ya Katiba na kufaa kwa dhana mbalimbali zilizoingizwa na kujengeka katika Rasimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kile ambacho Wajumbe mtaona kinastahili kuboreshwa au kurekebishwa au kufutwa msisite kufanya hivyo ili Watanzania wapate Katiba iliyo bora. Msipofanya hivyo kuna hatari ya kupata Katiba ambayo ni ngumu kuitekeleza. Aidha, tunaweza kuwa na Katiba ambayo itanung'unikiwa na watu wengi na kusababisha madai ya kutaka ifanyiwe marekebisho muda mfupi baada ya kupitishwa. Bunge hili linao wajibu maalum wa kuzuia balaa hilo lisitokee katika nchi yetu. Ngazi mbalimbali zilizowekwa katika mchakato huu ni kama chujio la kuepusha hali hiyo isitokee. Kile ambacho hakikuonekana katika hatua moja kitaonekana katika hatua inayofuata na kurekebishwa. Nawaomba fursa mliyonayo muitumie vizuri-RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, 21 MACHI, 2014, DODOMA
 
Mnahangaika sana na CCM iliyoshindwa kuwaletea maendeleo watanganyika kwa miaka zaidi ya 50. Imebaki na ahadi tu miaka yote, rais huyu huyu JK kadanganya eti "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania", Kustuka watz wanauziwa mafuta ya taa bei ya petrol etc.
 
al shabaab wenzake wametangaza kuhamishia vita kenya, huku kinana akizidi kuteketeza tembo wetu...
 
Amekwenda kwa MUUMIANI wenzake.

Jimbo la Iramba ndo wananchi wake wengi hawajui kusoma na kuandika.

Kuna uhaba mkubwa wa maji vijiji viingi.

Ugonjwa unaotesa wananchi ni TRAKOMA kutokana na Makazi duni.
 
Amekwenda kwa MUUMIANI wenzake.

Jimbo la Iramba ndo wananchi wake wengi hawajui kusoma na kuandika.

Kuna uhaba mkubwa wa maji vijiji viingi.

Ugonjwa unaotesa wananchi ni TRAKOMA kutokana na Makazi duni.

Makazi duni haisababishi TRAKOM ila kama makazi hayo yana mazingira machafu.
 
Ahh Jana kwa kweli Kinana amefunika! Mambo yalikuwa boraa sana na kwa kweli Singida kiboko!
 
Kinana ni JANGA LA TAIFA ni suala la muda tu ukweli wote kujulikana, Mara ndovu mara kampeni za CCM zinazohusishwa na wizi mkubwa wa fedha, hawezi kampeni meneja huyu kuwa safi hata dk moja.
 
Mwizi ni mwizi tu hata akiwa na cheo na wadhifa mkubwa kwa jamii. HUYU HUYU NDOVUMAN leo atatueleza nini??
 
Kinana amekuwepo Serikali hii ya Ombaomba tangu enzi za Mwanzo za Chama chakavu hakuweza kuwashauri,jahazi linazama ndio ataliokoa? Ni muda kila kitu kitakuwa wazi
 
Kumbe ukienda kwenye Jimbo la naibu katibu mkuu unakuwa na hofu ya kupata watu kiasi hiki, sasa hayo majimbo mengine hali iko je?
 

Attachments

  • image.jpg
    38.3 KB · Views: 222
Kwa hatia hii ukawa na washirika wao wakusanye virago vyao mapema kabisa hawana chao kwa majimbo yote ya tanzania.
 
Kumbe ukienda kwenye Jimbo la naibu katibu mkuu unakuwa na hofu ya kupata watu kiasi hiki, sasa hayo majimbo mengine hali iko je?
Wewe jifanye umechanganyikiwa lakini moto utakuwakia tu make unajifanya unajua kumbe unaungua jua ccm kiboko yako.
 
Huwa ninacheka sana wanapofanya maigizo ya kubeba tofali huku wakisubiri kupigwa picha,tanzania yangu nakupenda kwa moyo wote.
 

Kwa hiyo hasa tunakusudia kusemaje? Viongozi ndiyo wan akili kuliko wananchi? Au labda wananchi walikuwa hawajui wanataka nini wakati wanachangia hoja wakati wa ukusanyaji wa maoni?

Au nani atatoa kipimo cha nini kinafaa na nini hakifai kupita? ni viongozi walioonyesha tayari kushindwa kutekeleza katiba ya sasa na kuivunja kwa makusudi au?

Nadhani kimsingi kunakuwa na tatizo kama watu wengi wenye macho watakubali kuongozwa na vipofu wachache.
 
Kwa hatia hii ukawa na washirika wao wakusanye virago vyao mapema kabisa hawana chao kwa majimbo yote ya tanzania.

Tatizo ni ukawa au umaskini unaozidi kila uchao? Jimbo la iramba ni moja kati ya majimbo yenye umaskini sana Tanzania na mboga kuu hapa ni dagaa, wananchi wakiamka wanamkia mtukuru vilabuni! ccm wanatumia ujinga wao kufanya watakavyo, kama yupo mzawa wa Iramba humu atakua shahidi kwa chili.
 
Kinana ni JANGA LA TAIFA ni suala la muda tu ukweli wote kujulikana, Mara ndovu mara kampeni za CCM zinazohusishwa na wizi mkubwa wa fedha, hawezi kampeni meneja huyu kuwa safi hata dk moja.
Janga la taifa kwa mawazo yako.

Wimbo wa ndovu umeishapitwa na wakati. Tafuteni wimbo mwingine.

Ninyi mnafahamu vizuri kuongea, CCM tunatenda.

Karibu kwenye mkutano ujionee upendo na amani iliyoko ndani ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…