MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Sehemu ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiwa na Naibu Katibu Mkuu Mh. Mwigulu Nchemba katika maandalizi ya kumpokea Katibu Mkuu.
Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara akimpokea Katibu Mkuu CCM-Taifa Mh. Kinana alipowasili Jimboni Iramba kwa ajili ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Wilaya ya Iramba.
Katibu Mkuu akikaribishwa na wananchi kwa ngoma za asili.
Mwigulu Nchemba akicheza ngoma ya asili.
Katibu Mkuu CCM Taifa Mh. Kinana akishiriki na wananchi katika Ujenzi kwenye Kituo cha Afya cha Kaselya Jimboni Iramba
Katibu Mkuu Kanali Mstaafu Kinana akipanda Mti wa Kumbukumbu kwenye Kiwanda cha Kuchuja Alizeti Kata ya Ndago.
Hili ni jengo la Kituo cha Afya kata ya Shelui ambalo linajengwa kwa Nguvu za Wananchi wakisaidiana na Mbunge wao, Mh. Mwigulu NChemba.
Katibu Mkuu akijumuika katika ujenzi wa jengo hilo.
Mh. Mwigulu Nchemba akiweka sawa Zege kwenye Ujenzi wa Kituo cha Afya Shelui ambacho amechangia Mifuko 100 ya sementi kwenye Ujenzi wa Kituo hiki.
Katibu Mkuu akiwasili viwanja vya stendi Kiomboi katika mkutano wa hadhara.
Sehemu ya umati wa Wananchi wakionesha hisia zao za furaha mara baada ya Msafara wa Katibu Mkuu kuwasili Kwenye eneo la Mkutano-Kiomboi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Moses Nnauye akiwahutubia Wananchi wa Iramba-Kiomboi, Kubwa amesisitiza WanaCCM kuwa Wamoja kwasababu kuna baadhi ya Vyama vya Upinzani vinajenga mafarakano katika Taifa kwa malipo ya madaraka. Viongozi hawa wanadiriki mpaka kutoa matusi na dharau kwa waasisi wa Taifa letu ambao wamelijenga taifa linalowawezesha kupata nafasi ya kuingia kwenye bunge na kuanza kutukana na kukejeli juhudi za Wazee wetu.
Mwigulu akiongea na wananchi wapiga kura wake kuhusu mafanikio na mikakati katika utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo lake.
Mwigulu Nchemba na Nape Nnauye wakiwa kwa pamoja jukwaani.
Katibu Mkuu akiwa jukwaani na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mzee Msindai.
Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dkt. Parseko. V. Kone