Katibu CCM mbaroni kwa utapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu CCM mbaroni kwa utapeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Jan 28, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Akamatwa, alala kituo cha Polisi
  [​IMG] Adaiwa kutapeli magari 18, manne yakamatwa, mengine yasakwa
  [​IMG] Alikuwa anadai ni kwa ajili ya chama  [​IMG]
  CCM  Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, amekamatwa na polisi mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli magari 18 kwa kutumia jina la chama hicho.
  Magari ambayo Manara anadaiwa kutapeli, baadhi yanamilikiwa na watu binafsi na mengine yanamilikiwa na makampuni ya kuuza magari ya jijini Dar es Salaam.
  Kigogo huyo wa CCM Mkoa, ambaye pia ni mtoto wa mwanasoka mashuhuri wa zamani nchini, Sunday Manara, alikamatwa juzi kwa tuhuma hizo na kushikiliwa katika kituo cha polisi Magomeni hadi jana mchana alipotolewa kwa dhamana.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, alithibitisha kukamatwa kwa Manara na kusema kwamba, magari manne, ambayo anadaiwa kuyatapeli, yanashikiliwa katika kituo hicho na kwamba, uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea.
  Kalinga aliiambia Nipashe kuwa magari manne yanayoshikiliwa na polisi, yalikutwa kwa watu tofauti, ambako Manara anadaiwa kuyaweka rehani kwa kupewa mkopo wa fedha.
  Kamanda Kalinga alisema kuwa magari mengine 14 yaliyosalia, bado yanatafutwa na polisi.
  Kamanda Kalinga alisema kuwa kati ya magari, ambayo Manara anatuhumiwa kutapeli, 11 yanamilikiwa na mtu mmoja, sita mtu mmoja na moja linamilikiwa na mtu mwingine.
  Alisema wamiliki wa magari hayo, ndio waliowasilisha polisi malalamiko kuhusu utapeli unaodaiwa kufanywa na kada huyo.
  Kamanda Kalinga alisema kuwa katika tuhuma hizo, Manara anadaiwa kuwa alitapeli magari hayo kwa nyakati tofauti, baada ya kuwafuata wamiliki wake na kuwalaghai kuwa wanahitaji kuyakodi kwa ajili ya shughuli za chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana.
  Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi za mitaa, vitongozi na vijiji ulifanyika nchini kote Oktoba 25, mwaka jana.
  “Akikodi analipeleka gari kuweka rehani kwa mtu mwingine ili apewe pesa. Akipewa pesa, siku nyingine anarudi tena kwa mtu yule yule aliyempa pesa amuongeze pesa nyingine na aendelee kulishikilia gari husika,” alisema Kamanda Kalinga.
  “Katika upelelezi wetu, tulionana na uongozi wa juu wa CCM, lakini wamekanusha kuwahi kumtuma kwa shughuli hiyo. Wametwambia CCM wanayo magari ya kutosha,” aliongeza:
  “Tunafanya uchunguzi kubaini kama alikiuka sheria, kama itabainika kuwa alikiuka sheria, atachukuliwa hatua za kisheria.”
  Habari zilizopatikana jana, zinaeleza kuwa Manara aliachiwa na polisi jana mchana, baada ya Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu (CCM) kumchukulia dhamana katika kituo cha polisi alikokuwa akishikiliwa tangu juzi.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  siku zote nimekua natilia shaka uwezo na ujanja ujanja wa haji katika siasa, amekua nakipaji cha kupanda nafasi mbalimbali, sasa kwa hili ameumbuka, sasa kweli naamini CCM uimeoza, inanuka maana hawa vijana tuliodhani wanakuja kurekebisha mambo ndo wanaharibu kabisa.
  Haji anawakilisha makundi makubwa ya vijana wanaotirirkia CCM kusaka ngawila kwa njia za mkato, kukoomesha wezi wa kutumia nafasi zao ni kuung'oa mfumo wote, natuanze kwenye uchaguzi huu mkuu.....
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mtumeeeeeeeeeee.Manara!!
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ndivyo walivyo CCM wote, wewe ukiona kina Lowassa na mvi zao wanahomola mali ya Umma usitegemee watoto wao wataziachia.
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  big up haji manara!!

  sasa kama baba zako waliokufundisha siasa na wanaoendelea kukufundisha siasa wanafanya hivyo, wewe ulaze damu????????????

  sansana utakuwa mwanafunzi mbaya, sasa umeprove kuwa uko tayari kuhitimu, big up dogo
   
 6. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Haji I am so disappointed with u. Wakati unatafuta ukatibu mwenezi nilikupigia debe kweli kweli dhidi ya Wambura pamoja na kuwa Wambura alikuzidi personality. Nilipokuwa nauangalia uzeru uzeru wako na backaground ya baba yako mzazi na Baba yako mkubwa Kitwana Manara nikajua unafaa. Lakini baada ya kupata nilitegemea background yako ya uandishi wa habari ungeweza kuijenga CCM mkoa kwa kutake advantage ya taaluma yako na Radio Uhuru na Magazeti kama vile MZalendo na Uhuru ungeliwatumia ili kuijenga CCM. Sasa umethibitisha kabisa kuwa viongozi wengi wa CCM ni mafisadi na wezi. Wewe umekichafua chama inabidi na CCM ijisafishe kwa kuhakikisha unafungwa. Na huyo mbunge wa Ilala naye anakuwekea dhamana maana yake naye hafai ni fisadi. Ramesh Patel kwa nini usigombee Ilala?
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hata katika ukristo tunaamini kuwa dhambi ikikomaa huzaa mauti. Hakuna alichofanya manara kilichotofauti na yaliyotungwa ndani ya ccm. Haiwezekani kuanza kujenga uadilifu kuanzia chini. Unataka hawa kina manara waige kwa nani? tunaongea kiswahili au kisukuma kwa kuwa ndiyo lugha wanayoongea wazazi wetu. Alichokifanya Manara ndicho wanachofanya wazazi wake katika siasa! Anzeni kuilaumu ccm na sio kina manara ambao wanatokana na mfumo. Ulijenga imani nae kwa kuwa alikuwa nje wakati huo; alipoingia ndani siyo yule uliyemfahamu!

  Tutafanikiwa kuibadilisha Tanzania mapema iwapo viongozi wetu wa juu watakuwa wa kwanza kubadilika, kuipenda Tanzania na kuitumikia kwa moyo safi
   
Loading...