PreGE2025 Katibu ACT Wazalendo Songea, ahamia CCM

PreGE2025 Katibu ACT Wazalendo Songea, ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,573
Reaction score
2,496
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Wilaya ya Songea, Bi Grace Mallya, tarehe 19/5/2025 ametangaza rasmi kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza wakati wa kutangaza uamuzi huo, Bi Grace alisema ameamua kuhamia CCM kutokana na kuvutiwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Aliongeza kuwa ameshindwa kuelewa mwelekeo wa kisiasa wa ACT Wazalendo, hasa katika utekelezaji wa sera na mikakati ya maendeleo.

“Nimeona utendaji bora wa Rais Samia kupitia miradi mikubwa ya maendeleo na utulivu wa nchi. Hii imenishawishi kumuunga mkono kwa vitendo kupitia CCM,Kwa kweli, ACT Wazalendo haina mwelekeo wa moja kwa moja katika utekelezaji wa sera zake,” alisema Bi Grace.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM wa Manispaa ya Songea, Ndugu James Mgego, ambaye alipokea rasmi uamuzi wa Bi Grace, alimpongeza kwa hatua hiyo na kusema kuwa CCM kimeendelea kuwa kimbilio la Watanzania wengi kutokana na uongozi imara wa Rais Samia.

“Bi Grace amefanya uamuzi sahihi,CCM kimeendelea kuaminika kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchi nzima chini ya uongozi wa mwenyekiti wetu Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii ndiyo sababu hata viongozi wa vyama vya upinzani wanajiunga nasi,” alisema Mgego.
 
Dah, 2025 mtu kwa akili yake anahamia CCM

ambayo imeshindwa kutengeza uwanja wa Mkapa ili angalau tuione 5imba ikichukua kombe nyumbani!
 
Screenshot_2025-01-10-12-51-36-1.png

😆😆😆😂😂😂😂
 
Mallya!! nakumbuka Jiwe na Wachagga

Bwashe nigeshilingi!!
 
Back
Top Bottom