Katiba nyingi za nchi za Afrika hazina maana yoyote

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
227
597
Na Thadei Ole Mushi.

#Utofauti wa siasa zetu na za magharibi ni katika kuheshimu katiba za nchi tu. Pale Marekani mpaka ufikirie kuigusa katiba yao ni mpaka kuwepo na kitu hot kweli. Si rahisi uwaze kuigusa kwa kubadikisha kitu ndani yake na ukafanikiwa. Huku kwetu Africa ni jambo jepesi sana iwe wanachi wanataka au hawataki. MFANO:-

#Katiba ya Uganda inakataza raia yeyote wa Uganda kugombea kiti cha Urais kama miaka yake imeshavuka 75.

#Chama kinachoongozwa na Museven NRM kimepeleka mswada Bungeni ili kuondoa kipengele hicho ili Museven Agombee tena. Museven amekaririwa siku za karibuni kwenye Radio moja akidai kuwa wananchi waliowengi ndio wanaomuomba agombee.

#Huko Burundi Nkurunzinza amesema ataitisha kura ya maoni kupata maoni ya Wananchi kama agombee tena au aache nafasi hiyo. Amesema ataitisha kura hiyo siku za karibuni......

#Huko DRC Joseph Kabila amesema hana fedha za kuitisha uchaguzi nchini humo. Huu ni mwezi wa nane toka uchaguz huo uitishwe lakini haufanyiki.

#Kama wakifanikiwa kubaki madarakani watakuwa wameungana na wenzao Rais wa Equatorial Guinea Theodore Obiang Nguema, Rais wa Jahmuri ya Congo Denis Sassou Nguesso, Rais wa Rwanda Paul Kagame na Raisi wa Cameroon Paul Biya ambao tayari wameshafanikiwa kupindua katiba zao na watagombea hadi wachoke wenyewe.

KWETU TANZANIA

#Japokuwa si swala la kikatiba au si Swala linalogusa Katiba ya nchi moja kwa moja ila tumeshaanza kuwakaribia wenzetu hawa.

#Mwezi wa sita mwaka huu Chama cha Democratic Party(DP) kilimteua Georgia Mtikila kuwa MwenyeKiti wa chama hicho. Bi Georgia alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu kifo cha Marehemu mumewe Mchungaji Christopher Mtikila.

Chama hiki kiliendeleza yale yale yanayofanywa na vyama vingine vya siasa nchin. Undugu na kujuana ndio jambo ambalo linafifisha demokrasia nchini kuliko jambo lingine lolote.

#Haishangazi CCM kumuona mtu na mama yake au na baba yake bungeni. Si kwamba wote wamechaguliwa na wananchi lah hasha wengine kutokana na kujulikana kwao au ndugu yake alishatengeneza mazingira kwa wanaomfuata.

Nafikiri hili lipo wazi si mliona hata mchakato wa kupata wawakilishi wa bunge la Afrika mashariki? #Mimi ni mmojawapo ya watu ninaopinga nadharia ya kuwa uongozi ni wa kuzaliwa yaani kama baba kama alikuwa kiongozi mzuri haiwezi kugarantee na wewe kuja kuwa kiongozi mzuri.

Ni rahis sana kwa mtoto wa chenge aliyepo Sekondari kwa sasa kuja kukamata nafasi au hata kuwa mbunge kabla yangu mimi mwenye ndoto hizo 2020. Political Infrastructure walizonazo watoto wa viongozi si hizi tunazozidhani sisi.

#Chadema baba mkwe anamuachia mkwe chama. Na ukitaka kugombea unatimuliwa.... si mnaona hata viti vyao maalumu vinavyokwenda? Ukichaguliwa kupitia ticket ya viti maalum si kwa kuwa una uzoefu mkubwa lah Hasha lazma kuna mtu mbele mwenye nguvu ndani ya chama.

#Ni rahisi sana kwa mtoto wa Mbowe anayesoma sekondari sasa kuja kuchukua madaraka ndani ya chadema kirahisi zaidi kuliko Yericko Nyerere anayelima bamia huko mbutu.

#UDP Wao mpaka leo John Cheyo hajapata wa kumwachia Chama. Unamwachiaje chama mtu ambaye si wa damu yako? Huyu alikianzisha chama na atakufa nacho au labda aje atokee mtoto au mjukuu mwenye interest na Siasa.

#CUF Wao wanavurugana tu watu wale wale wanaamini kuwa wao ndio viongozi bora tu. Wangekuwa na nia njema wangengatuka wote na wakapatikana vijana wa kulisogeza gurudumu mbele... labda nao wanasubiri watu wenye vinasaba nao wawaachie chama.

Kwa ujumla Vyama vyote vimetumbukia kwenyetego huu. Sisi tuendelee kuvurugana kwa matusi na Mihemko huku mitandaoni.

Post hii niliiandika tarehe kama ya Leo 2017

MWAKA 2018 NAWEZA KUWAAMBIA NINI?

Katiba ni mkataba kati ya Wanaotuongoza na Sisi. Mkataba huu lazma uridhiwa na pande zote mbili.

Katiba ni utaratibu wanaojiwekea watu wa namna ya Kujiendesha.

Katiba mpya hutengenezwa kukidhi mabadiliko ya kijamii, Kisiasa na Kiuchumi.

Taratibu zetu za maisha zinapobadilika lazma tutengeneze utaratibu mpya wa kujiongoza.

Swala la Katiba haliamuliwi na viongozi pekee, ni mchakato shirikishi yaani jamii nzima mnakubaliana kwa matakwa au Kura za wengi tujiongozeje.

Taifa Lolote litakalokiuka utaratibu huu wananchi huwa hawaishi kunugunika na kulalamika.
 
Back
Top Bottom