Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mouhat, Aug 13, 2012.

 1. M

  Mouhat New Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tutambue umuhimu wa nafasi iliyo mbele yetu ya 'UTUNGAJI WA KATIBA MPYA' katiba tuliyo nayo ni ya miaka 50 iliyopita. mawazo na mazingira ya wakiti ule mbali ya kua yalikua ya wachache ya mfumo wa chama kimoja
  lakini yamepitwa na wakati. baada ya miaka hamsini tumeyaona yote ambayo hayana maslahi kwa taifi ,Taifa kwa maana
  ya wa-Tanzania. bila shaka katiba iliyopo sasa aidha kwa makusudi au kutokuelewa katiba hiyo ipo kwa maslahi ya wachache, nidhahiri wachache hao ni viongozi wa siasa waliopo madarakani, kama ilitungwa hivyo kwa makusudi, mungu ndio anajua.
  Siamini kua nafasi hii inaletwa kwa upendo wa viongozi wetu ambao wao ndio inaowanufaisha,ni upepo wa mabadiliko
  dunia inabadilika na ni lazima Tanzania pia ibadilike.nisipoteze muda niyataje yale ambayo ni lazima yabadilike katika
  katiba mpya
  a, Madaraka ya Rais ni mengi mno,rais asichague mawaziri kisiasa,awapendekeze kwa taaluma zao kisha bunge
  liwahoji na kuwapitisha likiridhia kua wanafaa.
  hii iende sawia ni uteuzi wa wakurugenzi na majaji.
  b, Nafasi za wakuu wa mikoa ziondolewa, hazina faida na zinaongeza matumizi ya fedha za wanainchi bila sababu
  na zinakwenda kinyume na katiba ya vyama vingi.
  c, Mgombea binafsi kwa nafasi zote ni haki ya kila mTanzania kugobea uongozi bila kufungamana na itikadi za
  chama chochote
  d, Tume huru ya uchaguzi.
  e, wanainchi wawe na mamlaka ya kumng'oa madarakani kiongozi yeyote wakati wowote endapo ataenda kinyume
  cha walio mchagua, hii itawafanya walio chaguliwa wawajibike badala ya jeuri ya miaka.
   
Loading...