mwanandugu
Member
- Mar 23, 2014
- 44
- 9
Kama tunataka kujenga muungano imara, tunapaswa kuwa na rais mmoja tu, yaani yule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Halafu kila upande wa muungano uongozwe na mawaziri wakuu. Mmoja aunde serikali ya Tanganyika na mwingine aunde serikali ya Zanzibar. Viongozi hawa watatu (yaani rais na mawaziri wakuu wawili) watachaguliwa na wananchi. Na watakuwa chini ya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya muungano.
Suala hili halitaizua Zanziba kuwa nchi kulingana na katiba yake. Nafikiri kwamba huu ndiyo mwarobaini pekee wa malumbano yanayoendelea katika bunge maalum la katiba mpya. Au mnasemaje ndugu zangu watanzania ?