Mjadala wa katiba mpya unapiganiwa na wanaharakati wa kisiasa wakishinikiza wananchi kuwaunga mkono, lengo lake kuu si kuwasaidia wananchi (wamachinga,mama ntilie, wafanyakazi) bali ni kuawasaidia wanasiasa hao kushika hatamu za uongozi kwa maslahi yao na familia zao, na pia kuongeza nafasi za uongozi, kuvunja muungano, kuifanya Tanzania kuwa nchi ambayo si salama kuishi, nchi ya maandamano.
Kuna vipengele vichache katika rasimu ya katiba ambavyo vinatolewa macho na wanasiasa kwa kushirikiana baadhi ya wafadhili wao wasioitakia mema nchi yetu ambapo wanaamini vikibadilishwa Tanzania itakuwa si nchi salama kuishi, nchi ya maandamano yanayopelekea watu wengi kuuliwa hovyo kama Kenya, nchi ya kuapishwa marais wawili kama Kenya, nchi isiyo na utulivu kwa wananchi wake kama, Iraq,Libya, Somalia, Syria, Palestina,Kongo, Nigeria, Sudan, Ethiopia na nyingine nyingi.
Wanaamini vipengele hivyo vikibadilishwa watavitumia kwa kuwashawishi wananchi kufanya fujo na maandamano ili wao walazimishe kupata uongozi baada ya watu kufa (si wao wala familia zao bali wamachinga, bodaboda, mama ntilie) huku wafadhili wao wakiamini fujo hizo zitawasaidia wao kuiba rasili mali zetu kama gesi , madini, wanyama pia watanufaika endapo kupitia viongozi hao wa kisiasa wanao watumia kuvuruga Amani ya nchi kwa kivuli cha demokrasia.
VIPENGELE PEKEE VYA RASIMU YA KATIBA WANAVYOPIGANIWA NA SABABU YA UHITAJI WA KILA KIPENGELE
Katika kipengele hichi muundo wa serikali, wanasiasa hawa wanalazimisha uwepo wa serikali tatu (3) badala ya mbili zilizopo sasa.
Serikali tatu(3) zina msaada gani kwa mmachinga na mwananchi mwingine? (hakina msaada wowote)
Kipengele hichi kiko wazi kabisa kudhihirisha malengo ya wanansiasa hawa kuwa wanachohitaji ni wao kutimiza haja zao za kiuongozi na si kumsaidia mwananchi wa kawaida.
Hakuna kipengele hata kimoja tofauti na hivi ambavyo utawasikia wakiongelea katika majukwaa yao.
NI Kipengele kipi kati ya hivi wanavyopigania kinagusa na kuleta unafuu wa maisha ya mtaanzania ya kila siku Zaidi ya kuuhadaa uma kwa maslahi yao, familia zao na vyama yao?
Tuwapinge kwa nguvu zetu zote , tusiwaunge mkono na badala yake tujikite kwenye shughuli zetu za uzalishaji kwa maslahi ya familia zetu na taifa letu.

- KIPENGELE CHA 73(4) KIMEBAINISHA NA KUSEMA,
“Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara hii,
Rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.”
Hichi ni kipengele mojawapo kinachopiganiwa na wasioitakia mema Tanzania.
Kipengele hichi kinamsaidiaje mwanannchi wa kawaida? (hakina msaada wowote)
- Wananchi hapo wametumika kama kinga na kukipa nguvu kipengele hiki, ila lengo kuu la kipengele hiki ni kumnyima mamlaka rais juu ya udhibiti wa vyama vya siasa vitakayoamua kuyafanya kuvuruga Amani ya nchi, kupitia kipengele hichi kutakuwa na maandamano kila siku na kazi hazitofanyika.
Katika kipengele hichi muundo wa serikali, wanasiasa hawa wanalazimisha uwepo wa serikali tatu (3) badala ya mbili zilizopo sasa.
Serikali tatu(3) zina msaada gani kwa mmachinga na mwananchi mwingine? (hakina msaada wowote)
- Lengo kuu la kudai serikali tatu ni kudhoofisha muungano wa nchi yetu na kuongeza nafasi za uongozi wa kisiasa, athari zake ni muungano dhaifu na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali ktokana na uwepo wa marais watatu na serikali zao.
Wanasisa hawa pamoja na wafadhili wao wanaamini kupitia serikali tatu rais wa jamhuri ya muungano hatokuwa na nguvu yeyote kiuongozi na hivyo kupelekea kuvunjika kwa muungano ili wao kushika uongozi (divide and rule) , hali hii itaifanya nchi yetu kukosa ushirikiano na umoja kama inavyotokea katika muungano wa visiwa vya Anjuan na mayote (Comoro) ambapo walimpindua rais sababu ya serikali tatu na Tanzania ndio iliwasaidia.