Katiba mpya ndio ukombozi wa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya ndio ukombozi wa watanzania

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by ismathew, May 25, 2011.

 1. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema ielekeze nguvu zake zaidi katika kufanikisha katiba mpya. haswa kuanzia vijijini mpaka katika mikoa yake. hili uwezekano wa katiba mpya uwe kabla Kikwete ajamaliza muda wake yaani ndani ya miaka mitatu. kwa sababu Kikwete anatambua wazi kuwa katiba mpya ndio mwisho wa ccm. na ndio maana analizungusha hilo jambo kufanyika haraka. Kwa kuwa kuna kila sababu za kikwete kuitwa Rais wa mwisho kutoka ccm. na jambo hilo ndilo linalomsumbua akili yake. Kama ccm imemfia mikononi mwake. Jambo la katiba lazima livaliwe njumu. bila hivyo udikteta utakuwa unaendellea tanzania. Miaka hamsini ya uhuru umeme hamna watu wanaumiiza vifua kwa moshi wa koroboi maendeleo yetu yanaenda katika mifuko ya watu wachache.Kwani maendeleo ya nchi ni maadili ya utendaji wa kazi. Kuhakikisha miradi yote pesa inatumika kihalali mpaka senti moja ya mwisho iliyopangiwa. Katiba sasa hivi si jambo la wananchi wote kufanya mchakato vipengele vya katiba.
   
 2. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vyema Mkuu ukaainisha ni Katiba ipi unayokusudia.

  Mimi ningeshauri mngeandaa kudai Tanganyika yenu na mkaiandikia Katiba yake maana sisi Wazanzibari ni mzigo kwenu.

  Wakati nyinyi mnalilia umeme, sisi tumesema wazi hata deni hatutolipa na hakuna lolote mnaloweza kufanya kwa kulinda "muungano" huu feki/

  Tatizo nnaloona ni siku mkaamka hakuna Tanzania wala Tanganyika maana Tanzania bila ya Zanzibar haiwezekani lakini Zanzibar bila Tanzania inawezekana.

  Amkeni Watanganyika, msiendekeze ufisadi tu na kuikalia Zanzibar kwa mabavu:

  haya tena basi jamani 3.jpg
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tulikuwa tunayaona Afrika Kusini wakati ule wa ukombozi, tuliwalaani sana makaburu kwa kuua waafrika. Leo hii Tanzania ya sasa serikali ya CCM ina-ua raia wake yenyewe kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

  [​IMG]
   
Loading...