kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 235
LAT huhitaji PhD kujua kwamba vyama vikubwa vya siasa ni CCM na CDM, sasa kilichobaki ni Muswaada tu wa kuua huu utitiri wa vyama vya matumbo vyote vijiunge na hivyo vikuu viwili na kuwepo na wagombea huru!
Willy badala ya kutumia rungu kuviua ni vyema kuongeza upana wa uhalali wa vyama vya siasa kuendelea kuwepo. Lets say kama chama cha siasa hakijapata uwakilishi ndani ya chaguzi mbili kuanzia udiwani na ubunge kiwe domant. Kusiwe tena na ruzuku kwa vyama vya siasa. Hakika yake vitakufa vingi vyenyewe na wanasiasa biashara watapotea wenyewe.
Mimi naunga mkono kufukuzwa uanachama wa mwanachama yeyote ndani ya chama cha siasa pale sheria na kanuni zote pamoja na haki na uwanja wa kukata rufaa mahakamni kuwepo ili asionewe mtu. Ila swala la kutokuwa na adhabu silikubali kwani binadamu huwa ananidhamu akijua hukumu.
Nchi zote zilizoendelea zinaheshimu sheria zao kwa sababu zinawashughulikia wote wanaozivunja bila kujali aliyezivunja ni nani. kama ingekuwa Tanzania Enron leaders wangekuwa mtaani kama walivyo wa EPA kwani tunaogopa kuwajibishana. Ningefurahi Kafulila angeenda mahakamani ili kumuumbua Mbatia au kujiumbua mwenyewe. Wao ni watunga sheria lazima wawe mfano.