Katiba mpya na Warioba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya na Warioba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Erasto..sichila, Apr 11, 2012.

 1. E

  Erasto..sichila Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya ni muhimu sana tuna katiba ya sasa tangu uhuru kwa takribani miaka 50 sasa hivyo ni kweli katiba inahitajika kunasheria nyingi za kikoloni zimepitwa na wakati hivyo katiba ni muhimu sana ,ndugu Warioba na tume ifanyekazi kwa niaba ya watanzania binafsi mwenyekiti Warioba ni mwaminifu na mtu mwenye uchungu nataifa hili haongeki kirahisi ni mwanafunzi wa mwl katika siasa za tanzania swala la tume kuwa na wajumbe nusu kwa nusu nikweli halina shida sana swala la waislamu wengi siyo shida ila hata wa wakristo wangekuwa wengi baadhi ya watu wengilalamika hivyoMtei hajakosa haki kuongelea hili ana hoja walio mkosoa hawana hoja na ni watoto ktk kufikiri mapendekezo yangu:1muungano uendee, kama ulivyo lkn raisi wa zanzibar awe ndiye makamu wa muungano,bilakujali chama chake 2kuwe na tume huru ya uchaguzi wateuliwe na bunge waombe nafasi zakazi na wapigiwe kura na wabunge wote3 madaraka ya raisi asiteuwe watu muhimu mfano jaji ,raisi asiwe na kinga akisha acha uraisi .4 kusiwe na wakuu wa mikoa na wilaya hizi ni nafasi za siasa zina haribu uchumi wa nchi 5wake na watoto za viongozi hasa raisi wajiingize kwenye siasa .ok tuendelee kutoa maoni
   
 2. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hebu tuangalie hapo kwenye red, mimi napenda kutofautiana na wewe kwenye swala hili.
  Tunakumbuka jaji Warioba aliongoza tume ya kumchunguza Waziri Nalaila Kiula mwaka 1996 kwa tuhuma za rushwa. Tume hii ilimhukumu Kiula bila ya kumpa nafasi ya kujieleza.
  Baadaye sana, katika kashfa ya Richmond ambayo ilipelekea waziri mkuu Lowassa kujiuzulu, jaji Warioba alimtetea Lowassa kuwa alihukumiwa na kamati ya Mwakyembe bila ya kupewa nafasi ya kujieleza.
  Katika maswala haya mawilitu, naona unafiki mkubwa sana wa Warioba. Yaani wakati yeye jaji Warioba alimhukumu Kiula bila kumpa nafasi ya kujieleza, hapo hapo jaji Warioba huyo huyo anamtetea Lowassa kuwa hakupewa nafasi ya kujieleza !!!!
  Maswali yanakuja:-
  • Kwa nini hakumpa nafasi ya kujieleza waziri Kiula ??
  • Kwa nini alimtetea Lowassa kuwa hakupewa nafasi ya kujieleza ??

  Huyu ndie jaji Warioba (Mwenyekiti wa tume ya Katiba !!!).
   
Loading...