Katiba mpya na ukubwa wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya na ukubwa wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KOMBESANA, Jun 23, 2012.

 1. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wana JF
  Singehitaji kupoteza muda kujadili gharama za Baraza la Mawaziri Tanzania kwa maana hilo liko wazi.
  Pia ni wazi kuwa kuna hatari ya baadhi ya Wizara kuingiliana kikazi,Wizara ya Ujenzi na ile ya Mawasiliano na Uchukuzi ziliwahi kugongana wakati wa kusafirisha vivuko, enzi ya Magufuli. Pia utaona kuwa Ujenzi kazi zake kubwa zinafanywa na TANROADS.Pia utaona kuwa kuwepo kwa Waziri wa Ulinzi, na Mkuu wa Majeshi ni DUPLICATION ya rasilimali na chanzo cha urasimu na hata migongano isiyo rasmi.
  Pia kwa kuwa KATIBA iko kimya kuhusu IDADI YA WIZARA,kila Rais ajaye kwa raha zake na kwa maslahi fulani anaweza kuongeza Wizara na kuzipunguza.
  Mjadala niliopendekeza hapa kwa wana JF NI HUU:
  k
  Kwenye nchi kubwa wenzetu wanafanyaje?
  Katiba iukiweka kikomo cha wizara miaka 50 ijayo ni vizuri?
  Wewe mwana JF mwenzangu hebu jaribu kutupatia kwa kadri ya uwezo wako wizara za serikali yako KIVULI na hoja za kuitetea
  Nawasilisha
   
Loading...