Katiba mpya na maoni ya wananchi

Katiba mpya na maoni ya wananchi

daniel merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
277
Reaction score
98
SEHEMU YA HOTUBA YA RAIS MWISHO WA MWEZI

Aliongeza:"Jambo lingine ambalo nimelifanya ni kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo. Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine. Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo."

"Rais Kikwete aliongeza kuwa na kwa bahati nzuri alitoa maoni yake mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba.


"Yangu yalikuwa maoni tu wana hiyari ya kuyakubali au kuyakataa
.
NIPASHE

Hapo juu ni sehemu ya hotuba ya rais. mimi nina maswali ya kujiuliza hivi wakati tume inakusanya maoni ilisahau kumhoji rais ambaye ni mkuu wa nchi mpaka aende kutoaa maoni yake ndani ya bunge wakati muda wa kutoa maoni ulikuwa umeishapita?

Je rais alikuwa sahihi kutoa maoni yake bungeni badala ya kutoa maoni kwa tume ya katiba?

Kwa maelezo ya rais kwenye hotuba anasema mahala alipotolea maoni ni sehemu sahihi kabisa.. swali langu mbona sisi wananchi wengine hatukuruhusiwa kutoa maoni yetu sehemu hii sahihi kama rais anavyosema kwenye hotuba yake? Je wengine tulitoa maoni yetu kwa kificho?

Au ndo kusema wengine wako juu ya sheria.

Naomba kama kuna mjumbe wa tume anasoma uzi huu anipe majibu au ufafanuzi wa maswali yangu hapo juu

SOURCE- NIPASHE
 
Nilifikiri aliitwa bungeni kufungua bunge, kumbe alienda kutoa maoni yake!?
 
Pale palikuwa ni sehemu ya kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa Bunge Maalumu na si sehemu ya kukusanya maoni ya raia. Rais kama ni raia nambari moja angeenda kwenye eneo la karibu na anapo ishi Tume ya Warioba ilipokuwa inakusanya maoni. Mbona kwenye kupiga kura huwa hapigi kura siku ya kutangazwa matokeo? Usanii kila sehemu!
 
Back
Top Bottom