Ndugu Nsimba;
Hakuna suala la kupiga tena kura miongoni mwao, inaweza kuleta rushwa/ufisadi ambao hatutaki kuisikia. Iko hivi:
Diwani akishachaguliwa, automatically ni mbunge, anasubiri mwaka wake wa kuliwakilisha jimbo ufike kutegemea kata yake/jina lake ni la ngapi kwenye mtiririko (alphabetical order). Endapo jimbo lina kata tano (na hivyo madiwani 5), utaona kila kata ina nafasi ya kuliwakilisha jimbo bungeni katika kipindi cha uhai wa Bunge (miaka 5) kwa sababu Diwani anawakilisha kwa mwaka mmoja tu unaofuata jimbo linawakilishwa na kata inayofuata.
Endapo kata ni pungufu ya tano, utaona kuna uwezekano wa ile kata iliyoanza kuliwakilisha jimbo kurudia. Baadaya ya uchaguzi mwingine, zitaanza zile kata ambazo zimewakilisha mara moja tu.
Endapo kata ni zaidi ya tano, utaona baadhi ya kata hazitapata nafasi katika ule mzunguko wa kwanza; hizi ndizo zitakazoanza uwakilishi Bunge linalofuata.
KUMBUKA: Hapa sizungumzii watu, nazungumzia Kata ambazo hudumu milele lakini watu (madiwaji kwa nafsi zao) huja na kupita.
Kwamba ili liwe "practical" bado siamini kwamba madiwani wetu ni mbumbumbu kwamba lazima wawe na sifa za juu sana kielimu. Ndugu yangu, katika suala la uwakilishi kinachotakiwa ni UZALENDO tu na si vinginevyo - hivi huoni wanaotusumbua sana nchi hii ni wasomi mahiri ambao wamegeuka badala ya kuwa na tabaka la wanyonge wamejitumbukiza kwenye ufisadi usiomithilika? Hata hivo kama profesa akiamua kwenda kugombe udiwani mimi sina tatizo na hilo - tuepuke kuweka majitu bungeni kwa muda mrefu (miaka 5) badala ya kuwa msaada yanageuka kuwa mizigo na kero.
Nakubaliana na wewe (na hata ndivyo wananchi wengi wanavyotaka) kwamba waziri asiwe diwani (na hivyo mbunge). Hakuna mduara a milele hapa, miaka mitano ikiisha ni uchaguzi kama kawaida halafu kata husika katika jimbo zinajipanga tena (hata kama kuna mpya iliyoongezwa) ni nani aanze kuliwakilisha jimbo kwa mwaka wa kwanza, vivyo hivyo wa pili, tatu, n.k hadi uchaguzi mkuu mwingine.
Pia faida nyingine ya mfumo huu ambayo sikuitaja awali ni kwamba tofauti na ilivyo sasa ambapo pesa zinatumika kwenye chaguzi ndogo pindi mbunge anapokosa sifa za kuwa mbunge, kwa mfumo unaopendekezwa hapa uchaguzi mdogo ni wa diwani tu ambao hauna gharama kubwa.
Hebu tuachane na kasumba za ku-copy kila kitu kutoka magharibi, hata mfumo wa kuendesha nchi yetu wenyewe? Kama wazee wetu kina Kimweri, Mkwawa, Isike, na watemi wengine wa nyakati hizo waliweza, kizazi hiki kinachojidai kimeendelea kinashindwa nini? Kama kusoma ni kunakili kila kitu, heri kutokusoma.
Nawasilisha.