mshaurimkuu
Member
- Jan 23, 2011
- 57
- 30
Ndugu Watanzania na wote wenye mapenzi mema kwa nchi yetu; Salaam.
Kutokana na matatizo mbalimbali ya bunge letu hasa haya yafuatayo:-
(i) Asilimia kubwa ya wabunge kujiona kuwa ni wamiliki wa majimbo wanayoyawakilisha ikishadidiwa na mfumo wa hovyo uliopo ambapo ni rahisi watu kupita kwa rushwa.
(ii) Asilimia kubwa ya wabunge kukimbilia Bungeni si kwa ajili ya uwakilishi wa dhati bali kufuata mishahara na posho nono.
(iii) Asilimia kubwa ya wabunge kutoonekana/kutoishi katika majimbo/maeneo yao ya uwakilishi.
(iv) Uwezekano wa kuwakilishwa na mbunge ambaye mchango wake si mzuri - kusinzia tu bungeni kwa MIAKA MITANO.
Kutokana na hilo, nashauri Katiba ijayo iwe hivi:-
(i) Kusiwe na nafasi ya kugombea kwenye uchaguzi inayojulikana kama Mbunge.
(ii) Badala yake kuwe na MADIWANI tu.
(iii) Madiwani wa jimbo husika wawe pia ndio wabunge wa jimbo hilo.
(iv) Diwani atawakilisha Jimbo Bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja tu kwa mzunguko yaani, kwa mfano kama jimbo lina kata labda saba, kila Bunge jipya linapoanza, Majina ya Kata yapangwe ki-alfabeti.
(v) Diwani wa kata ya kwanza (au ya mwisho kadiri itakavyoonekana inafaa) atawakilisha Jimbo Bungeni kwa mwaka wa kwanza. Utaratibu mwingine mzuri pia wa kupanga Kata ipi ianze uwakilishi unaweza kutumika (kama kupanga majina ya Madiwani ki-alfabeti, kuchagua jina kwa mfumo wa nasibu, n.k.).
(vi) Mwaka wa pili, atafuata diwani wa kata ya pili, hivyo hivyo hadi kata tano za kwanza ziishe.
(vi) Uchaguzi mkuu utakaofuata; wataanza madiwani wa zile kata ambazo hazikuwakilisha jimbo msimu uliopita hadi ziishe halafu tunaanza tena mwanzo - KITU KAMA MDUARA HIVI.
MANUFAA YA MFUMO HUU:
(i) Utaongeza ushirikishwaji zaidi wa wananchi kwani kila kata itawakilisha jimbo badala ya ilivyo sasa ambapo inawezekana mbunge mmoja kutoka eneo moja tu kuwakilisha jimbo kwa hata miaka 30!
(ii) Matumizi mazuri ya rasilimali: Hakutakuwa tena na kitu kinachoitwa gari la mbunge kama mtu binafsi bali gari la mbunge kama ofisi; mwaka ukiisha, gari linakabidhiwa kwa mwakilishi anayefuata.
(iii) Kuwa karibu zaidi na wananchi: Kusema ukweli wabunge wengi wa sasa hawaishi majimboni lakini madiwani wengi wanaishi huko hivyo wanajua vizuri sana shida na matatizo ya maeneo yao kuliko mbunge kwa mfumo wa sasa.
(iv) Mgawanyo mzuri zaidi wa mapato/keki ya taifa: Badala ya wachache kugawana kidogo kilichopo, angalau wigo unaweza kupanuliwa wakapata wengi yaani MARA TANO ZAIDI.
VIKWAZO:
Najua "wasomi" na viongozi wetu wengi wamekariri mambo ya wenzetu huko duniani na kudhani ndio amri au unabii kutoka kwa Mungu ambayo hakuna awezaye kuyabadili. Huwa nachukia sana unapomsikia mtu fulani mkubwa akisema "... tumerithi mfumo wa Westminster na ndio unaoutumika kuendesha Bunge letu". HIVI HATUWEZI KUWA NA KITU CHETU WENYEWE? Kwanini wenzetu wasiige kwetu badala ya sisi ndio wa kuiga tu? Hebu tujaribu mfumo wetu wenyewe maana hii ya wenzetu inatuletea tu matatizo.
Tafadhali jibu kwa hoja.
Naomba kuwasilisha hoja.