Katiba Mpya ihusishe haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya ihusishe haya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MPAMBANAJI.COM, Sep 7, 2012.

 1. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Pongezi kwa Serikali na tume ya Katiba Mpya

  Katika hitimisho la Katiba naomba na haya yazingatiwe:

  1.Wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi kila baada ya miaka mitano wakati wa uchaguzi mkuu na asiwe katika mfumo wa chama cha siasa

  2.msajili wa vyama vya siasa naye achaguliwe na wananchi wakati wa uchaguzi mkuu kila mara bada ya miaka 10 na sio Rais kama ilivyo sasa

  3.Siku ya Ijumaa iwe ni mapumziko na kazi zote za kiofisi zianze saa 1:30 asubuhi hadi 11 jion ili kufidia siku ya Ijumaa ila jumamosi ni siku kama kawaida

  4.Ikubalike japo Tanzania haina dini bali Bunge na shughuli zote za kiserikali zianze kwa sala ya jumla na kufungwa vivyo hivyo bila kutaja aina ya Mungu au mtume au Mkombozi Yesu.

  5.Rais atakayeshinda ni yule tu atakayefikisha asilimia hamsini na kuendelea ya kura zote

  6. Idadi ya vyama vya siasa viwe 6 tuu, ili kupunguza ukiritimba wa vyama, kuepuka migogoro ya maslahi kisiasa na pia gharama za kuendesha chaguzi mbalimbali.

  Haya ndo yangu kwa sasa wadau
   
 2. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,187
  Likes Received: 1,538
  Trophy Points: 280

  kwanza nianze kwa kusema nadhani maoni ungepeleka katika tume ya katiba kulekwenye web yao kuna e mail ya ku post
  pili cjaelewa kwanini ijumaa? na jumamosi ni siku ya kawaida? kivipi? hujaeleweka
  Tatu, bunge hapo, cjui kama huwa unackiliza Bunge, kwani huwa linataja imani flani? au yesu au mohamad (kumladhi kama nitakuwa sijaandika sahihi jina la huyo bwana)mi ninachochua huwa wanataja mwenyezi mungu baaasi au unataka waongeze na neno mizimu ya mababu?
   
 3. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Sawa kwa maoni yako. pia copy na kupest kwa e-mail yao

  1.Ijumaa ni vyema ikawa hivyo kwani minong'ono tayari imeanza kwa siku hii kutambulika rasmi kwa waislamu kama ilivyo Jumapili kwa Wakristo
  2.Juamosi huwa ni nusu siku kikazi kwa baadhi ya Ofisi hivyo iendelee hivyo hivyo
  3. Kusuhu sala..tayari maoni ya Tanzania kuwa na dini imeanza na ni vyema ikaendelea kama ilivyo sasa
  4. Kuhusu Yesu umemtaja vizuri na huja kosea

  Pia sina mrengo wowote wa kidini kwa kusema hya
  Aksante kwa maoni yako ila naogopa kutaja hilo jina laoko kwani nitakuwa nimekuballi we ni dumelang
   
Loading...