hapa kwetu umesoma hujasoma bado utakuwa kiongozi
Mkuu naomba nitofautiane na wewe. Kama unamaanisha kiongozi bora basi sifa ya kwanza, kama tukizipanga kwa mtiriko wa umuhimu, ya kiongozi bora sidhani kama ni kiwango chake cha elimu. Nadhani kuna sifa za kwanza na za muhimu kuliko elimu.
Wala kuwa na kiongozi aliyesoma sana kwangu sio la muhimu sana hadi masuala mengine pia yamezingatiwa. UONGOZI unahitaji sifa nyingine za ziada zaidi ya usomi vingenevyo hugeuka UTAWALA.
Nikupe mfano: Hivi karibuni (nadhani umesikia) UTAWALA wa UDSM uliojaa wasomi wa kiwango cha juu kabisa ulivyoamua kuwafukuza "forever" wanafunzi kadhaa tena kwa masharti eti hawaruhusiwi kudahiliwa (admitted) kwenye chuo kingine chochote nchini. Ukilitazama hili suala hata Kikatiba sidhani kama ni sahihi. Huu sasa ni UTAWALA na sio UONGOZI pamoja na usomi wao.
Watu wanashabikia shabikia tu hata upuuzi wanashabikia tu!! Hivi hamuoni kuwa katiba hiyo ni ya kijuha kama walivyo majuha wakenya wengi. Inakuwaje eti waziri awe professional halafu polisi igp anayesimamia amani na usalama wa raia asiwe na profession. Upu....mbafu mtupu baadhi mnashabikia tu shhiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit!