Katiba Iweke Wazi Mambo Haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Iweke Wazi Mambo Haya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Anko Sam, Jan 30, 2011.

 1. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa mapendekezo yangu Katiba Mpya inatakiwa iweke wazi mambo yafuatayo:-

  Hapa ni kwa nafasi za Urais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakurugenzi wa Wizara/Mikoa na Wilaya, Mkuu wa Mkoa/Wilaya, Wabunge, Madiwani,

  1: Katiba itamke upatikanaji wa kiongozi huyo.
  -Je, niwakuchaguliwa au niwakuteuliwa ama wakuomba kazi kwa barua!
  2: Itoe Madaraka na Mamlaka kwa kiongozi husika:
  -Mipaka ya Madaraka, Mamlaka na Uwajibikaji wake uainishwe kwenye kitabu
  kingine kitakacho chambua na kuweka mipaka ya utendaji wake. (Maadili nayo
  yawe humo)
  2: Katiba iweke muda maalumu wa kiongozi huyo kukaa madarakani.
  -Awe na ukomo wa vipindi au la.
  3: Katiba iweke WAZI jinsi ya kumuondoa Madarakani kiongozi huyo.
  -Kama atakuwa amevuja kifungu chochote cha Katiba hiyo au Kiapo chake.
  -Kama atakuwa ametuhumiwa au kutenda kosa lolote la jinai.

  Kwa hiyo kuwe na katiba na vitabu vingine vitakavyo kuwa na nguvu ya kisheria vikielezea kwa undani vifungu vya Katiba Mpya.

  Wananchi nao haki zao za msingi na wajibu wao kwa Taifa zitatamkwe na kutambuliwa na Katiba Mpya.
  1: Haki ya kuishi kwa Raia Mwema
  - Kama Mtu akivunja haki ya mtu mwingine, kama kuiba, kuumiza mwili, kutishia
  nk, mtu huyo anstahili naye haki zake zivunjwe!
  2: Raia awe na haki ya kuchagua ama kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa.
  - Asilazimishwe kujiunga na genge fulani la kisiasa ndiyo achague ama
  kuchaguliwa kuwa kiongozi wa jamii husika.
  3: Raia awe huru kuandamana ama kukusanyika na kujadili mambo yao bila
  kubughudhiwa.
  -Kama jamii moja ina amua kwa pamoja kukusanyika na kuandamana kwenda
  kwenye eneo la kuzungumzia, wawe huru na wasizuiliwe kwa namna yeyote ile.

  Mihimili ya Dola, yaani Serikali, Bunge na Mahakama visi-ingiliwe katika utendaji wake. Ila Bunge ndo sauti ya wananchi liwe na MAMRAKA ya kuhoji utendaji wa mihimili mingine.
  1: Bunge kwa sababu ni Chombo cha uwakilishi wa wananchi, kitachagua Spika wake.
  -Waziri mkuu awe ni kilanja wa shughuli za Serikali bungeni, yaani awe kiongozi wa
  mawaziri na makatibu wakuu kuweka mambo sawa serikali inapo banwa na
  wabunge. Asiwe mtu wa kuwa kolomea wabunge na kuwapa majibu mepesi kwa
  maswali magumu.
  2: Rais atapendekeza majina ya Majaji wa Mahakama Kuu/Rufaa wakathibitishwe
  na Bunge (Wananchi).
  -Bunge ndilo litakuwa na madaraka ya kumuondoa Jaji akionekana hatendi haki.

  Vyombo vingine vya maamuzi kama TUME HURU ya Uchaguzi, iwe na wajumbe kutoka kwenye taasisi zinazoheshimika ziwe za kidini, kijamii, Senior citizens, Wanasheria nguli, wanaharakati wa makundi yote nk nk.

  Naomba kuwasilisha!
   
 2. N

  Nyang'oma Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono yote uliyopendekeza kuwemo katika katiba. Jambo jingine ni kuhusiana na masuala ya serikali za mitaa. Mameya na wenyeviti wa halmashauri zote wachaguliwe na wananchi katika maeneo husika. Ni mameya na wenyeviti hao wakiwa pamoja na madiwani wao watachagua wakurugenzi au city managers tofauti na ilivyosasa wanaletwa kwa kuteuliwa na either waziri mkuu au waziri wa tawala za mikoa. Vile vile nadhani wakati umefika kuangalia entitlements za rais aliyeko madarakani na waliokwishastaafu. Gharama za kuwatunza hawa mabwana ni kubwa mno na wakati huo tunaona hali halisi ya mahospitali yetu. Mpango wa kumjengea rais nyumba kila rais ni upuuzi mtupu. Ikumbukwe kuwa wanapokuwa ikulu serikali inawanaghalimia kila kitu yaani chakula mpaka mavazi.
   
 3. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Naomba niongezee yafuatayo:

  3. Muundo wa wizara pamoja idadi ya wizara na mawaziri iwe ya kudumu kwa muda mrefu, badala ya kubadilisha badilisha kama hivi sasa.
  4. Vision ya nchi iwekwe wazi na isiwe mali ya chama kimoja. Kama ni kuwa na taifa la ujamaa au ubepari, iwe ni lazima kwa vyama vyote au kiongozi yeyote atakaye kuja madarakani, kuitekeleza vision hii. Vyama na viongozi wanaweza kutofautiana tu katika missions na mikakati mbali mbali katika kuifikia vision. Isiwe kila kiongozi anakuja na mambo yake na kufuta ya kiongozi aliyemtangulia. anayekuja
   
Loading...