Kati ya supu zote unapendelea ipi?

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,546
1,663

Binafsi napenda sana supu ya samaki tena napenda kuagiza kichwa maana bila ya kula jicho sijajickia kama nimekula.

Lakini pia kama hakuna napenda supu ya bata huniburudisha kwa radha yake kama hutotokwa jasho basi una matatizo kiafya. Haiishi hamu unatamani uendeleeeeee.

Wewe unapenda ipi?
 
Supu ya ulimi wa ng'ombe, aisee ni tamu...weka na pilipili kiasi, nikiwa Dar naipata leaders club everyday au pale karibu na ultimate security kinondoni.
 
Nyie wote mmepotea njia SUPU YA GOGO LA BUCHANI ile ndo mwisho wa yote, hasa liwe lina experience ya kama miaka 5 na zaidi maana nyama tofauti tofauti zimekatwa juu yake, sikui kikombe, sijui nundu sijui mbavu so ile mixer yake halafu lile gogo likachemswa huo mseto wake balaaaa hahahahahahahahahahahahahahah
 

aisee supu ya sikio la nyati ni balaaa.tena mpishi asipoweka chumvi nyingi na ndimu badala ya limao,lazima ujilambe .
 
Supu zote nimetumia, lakini SUPU YA MAWE ni kiboko. Mpaka utenzi nilitunga:

Supu ya mawe,
Ni supu kiboko,
Haina mfanowe,
Haina ukoko,
Hutia kiwewe,
Hulii kijiko.
 

Hivi unaongelea supu au vitu vingine [samaki,jicho,bata] ???
 
Kama ni supu ya kawaida na si mafumbo basi supu ya pweza ndio nambari one na nikiwa mwanza huwa napenda supu ya sato pale fisherman's hotel mwaloni.
 
If we are really talking about supu haijalishi ni mapishi tu..., kwa ajuae kupika hata supu ya mawe utaipenda...
 
Kweli JF imekuwa kubwa... Longtime sijakuona...., hope you are fine naona tuko jamii moja ila tunapishana tu... vibaya hivyo...:A S embarassed:

ooohh dear
samahani sana mpendwa..
si wajua tena mie ndo lawyer maeneo haya..
kazi imenizidia dear hahahahahah lol

we waendeleaje mpendwa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…