Kati ya mwanamke na mwanaume nani anapenda kudukua mawasiliano ya mpenzi wake na kwanini?

Nikijisemea mimi binafsi. ..wanaume ndio wa kwanza ....

Sababu wanazijua wenyewe...

Inawezekana hawajiamini kama kweli huyu mrembo ni wake peke yake?
Au ni katabia tu walichonacho. ..

Ila yote yanatoka na kwamba wenyewe hawajatulia na wana wasiwasi na demu hajatulia vile vile.
 
hello wana JF,

ningependa kujua kati ya wanaume na wanawake ,nani wanaongoza kudukua mawasiliano ya wapenzi wao.........................? kwa nini....??
Kwa kuwa Mimi ni mwanaume ninavyojijua Mimi ndio tulivyo wanaume wengi tunaongoza kwa kudukua mawasiliano .
Sababu zipo nyingi sana mf wivu wa mapenz,kuhisi hatia Fulani juu ya mambo ninayoyafanya na yeye anafanya hayo hayo n.k
 
Asanteni wote,naona jibu nimepata kuwa ni wanaume na sababu iliyojitokeza ni guilty kufikiria anayoyafanya ndio mwenzie na yeye anafanya,mengine ningependa muongezee lol
 
Siwezi kudukua simu ya mpenzi wangu bila sababu maalum, kwa mfano mabadiriko flani katika tabia yake hata yawe kidogo kiasi gani, lazima nifuatilie! Otherwise, no need!
 
Wote wanaulingano sawa, inatemegea tu ,

Mwenye mapenzi zaidi ya mwenzake ndio huwa anadukua ya mwenzie, sio kwa nia mbaya , msiwalaumu wanaodukua, binafsi nawaunga mkono wadukuaji, ni kwasababu yakujihakikishi usalama wa mapenzi yake kwa mlengwa
 
Mapenzi ya kibongo yamejaa usanii na unafiki sana, mi naweza sema ni mmojawapo katika hio tasnia ya udukuaji na nimtu wa kwanza kuwapa ujuzi huo baadhi ya members humu mapema sana kuhusu ile njia pendwa ya MTFV.apk

Inasaidia kujipanga na next moves mapema maana ukishaona mpenzio anapanga maisha na mwanaume mwengine ilihali akija kwako anakuita baby vilevile na manjojo kibao ujue kuna walakini tayari. Ni rahisi sana kumkamata mtu kwa cheating anazofanya akihisi we ni zuzu labda.

Na sio kila anaefanya udukuzi ni kicheche, mie sina tabia hio na nampenda sana mpenzi ninayekuwa nae kwa kipindi chote bila kumchoka. Ila kiukweli wanaume tuliotulia ndio wahanga wakubwa sana wa mademu wanafiki. Unakuta unamuamini mtu sana ila anaishia kuku dissapoint vibaya mno sasa ili kuondoa dissapointments naona bora nikudukue nikishaona dalili za unafiki nakupiga chini. Sitaki mazoea!
 
Back
Top Bottom