Kati ya Makonda na Nape nani anahitajika sana kimkakati na Magufuli?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Kwa siku za hivi karibuni nimeanza kuona Mheshimiwa Rais JPM akiwa anavutiwa mno na Utendaji wa hawa Wateule wake wawili Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mara nyingi amekuwa akiwataja na kuwasifia interchangeably kitu kinachothibtisha kuwa anawapenda na kuwakubali wote wawili.

SWALI.

Kwa manufaa ya Serikali na Chama Tawala ni nani pengine Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anamuhitaji sana Kimkakati hasa kuelekea kujipanga kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020?

Naomba kuwasilisha na nitashukuru kwa michango yenu.
 
Kama akirudi shule na kupata cheti na kuanza kutumia jina lake la halali, yeye na jpm wanaendana sana namna wanavyofanya maamuzi na jinsi wanavyoangalia changamoto za wananchi.

Ni dhahiri huyu yupo kwenye mikakati ya JPM ya muda mrefu kushinda huyu mwingine ndiyo maana wameshabihiana hivyo vitu ama kwa makusudi au ilidhamiriwa.
 
Wakati wa uchaguzi kati yao nani alifanya nini kumsaidia JPM kushinda? Jibu la hapo litaamua.
Maashallah jibu limenigusa
 
Nape atabaki kuwa mwokozi wa Chama!
Lakini pia,tumpe Makonda nafasi ya kujizihirisha zaidi utendaji wake!
Kwani ukiacha kashfa yake ya vyeti Makonda ni kijana Mzuri!
Ni jasiri,mfuatiliaji na asiyekubali kushindwa katika lolote!
Naona anaweza fika mbali katika awamu hii,na hata kuwa mrithi wa Magufuli come 2025!
Ila kwa sasa mpaka 2020 Nape ni wa Muhimu kivyote ndani ya Chama!
 
Yes, Lkn kabla hatujampa nafasi hiyo, tunataka kwanza authibitishie umma kwaba yeye si Daudi Bashite....to be trusted, you have to win people's trust.
 
Nape atabaki kuwa mwokozi wa Chama!
Lakini pia,tumpe Makonda nafasi ya kujizihirisha zaidi utendaji wake!
Kwani ukiacha kashfa yake ya vyeti Makonda ni kijana Mzuri!
Ni jasiri,mfuatiliaji na asiyekubali kushindwa katika lolote!
Naona anaweza fika mbali katika awamu hii,na hata kuwa mrithi wa Magufuli come 2025!
Ila kwa sasa mpaka 2020 Nape ni wa Muhimu kivyote ndani ya Chama!
Na pia anetengeneza historia tangu tupate Uhuru hakuna kiongozi aliye kuwa anawadhalilisha watendaji wa chini yake kama Makonda tena kwenye mikutano ya hadhara kwa mfano weka ndani huyo wewe ndiyo vichaa wanaotafukwa nk. Bila kujali umri wa mtu. Yeye ndiyo polisi yeye ndiyo kila kitu hakuna mgawanyo wa kazi. Nchi zilizoendelea zimefika zilipo fika kwa sababu kiongozi akichagua cabinet yake kila mtu anafanya kazi yake hamna mtu anafanya kazi isiyo muhusu.
 
Kama akirudi shule na kupata cheti na kuanza kutumia jina lake la halali, yeye na jpm wanaendana sana namna wanavyofanya maamuzi na jinsi wanavyoangalia changamoto za wananchi.

Ni dhahiri huyu yupo kwenye mikakati ya JPM ya muda mrefu kushinda huyu mwingine ndiyo maana wameshabihiana hivyo vitu ama kwa makusudi au ilidhamiriwa.
Hicho cheti atakipataje wakati anapaswa aende kwanza jera miaka 7, alafu aende aanze form 1 hadi aje kumaliza sekondari JPM atakuwa bado raisi?
 
Nape atabaki kuwa mwokozi wa Chama!
Lakini pia,tumpe Makonda nafasi ya kujizihirisha zaidi utendaji wake!
Kwani ukiacha kashfa yake ya vyeti Makonda ni kijana Mzuri!
Ni jasiri,mfuatiliaji na asiyekubali kushindwa katika lolote!
Naona anaweza fika mbali katika awamu hii,na hata kuwa mrithi wa Magufuli come 2025!
Ila kwa sasa mpaka 2020 Nape ni wa Muhimu kivyote ndani ya Chama!

Kwa vyeti vya kununua??
 
Wakati wa uchaguzi kati yao nani alifanya nini kumsaidia JPM kushinda? Jibu la hapo litaamua.
Nape siyo mvumilivu, pia Nape hana kipaji cha kupendwa na watu, yaani Nape siyo leader! Nape ni msema ovyo.

Siasa zetu kwa sasa ni za kufurahisha watu, yaani wakati mwingine hazihitaji upayuke kama Nape, bali zinahitaji mtu anayetatua matatizo ya watu. Hivyo kimkakati Nape hafai, Makonda anafaa kwa sababu wewe pita mitaa ya Dar kila mtu anamuongelea Makonda kuwa jiji kaliweza na wanafurahi sana wana dar
 
Kwa siku za hivi karibuni nimeanza kuona Mheshimiwa Rais JPM akiwa anavutiwa mno na Utendaji wa hawa Wateule wake wawili Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mara nyingi amekuwa akiwataja na kuwasifia interchangeably kitu kinachothibtisha kuwa anawapenda na kuwakubali wote wawili.

SWALI.

Kwa manufaa ya Serikali na Chama Tawala ni nani pengine Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anamuhitaji sana Kimkakati hasa kuelekea kujipanga kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020?

Naomba kuwasilisha na nitashukuru kwa michango yenu.
Mkuu GENTAMYCINE, dawa inayotibu magonjwa mengi yaambukizwayo na bacteria, jibu langu ni Makonda.
Kwa sababu:
Siasa zetu kwa kizazi hiki zinahitaji kiongozi anayetatua kero za watu wengi, ambapo Makonda hicho kipaji anacho, tofauti na Nape ambaye ni mropoka ovyo tu. Nape hana uwezo wa kushawishi, ila Makonda uwezo huo anao na tena kwa kujenga hoja. Wewe chukulia mfano suala la madawa, mimi nina ushahidi watu wengi dar wamekuwa wakipiga Magoti kumuombea ulinzi kwa Mungu Makonda kwa ujasiri wake wa kuwataja wauza madawa (katatua matatizo ya wengi), wakati huo huo Nape anakuja kusema kuwataja hadharani ni kosa (anawafurahisha wauza madawa wachache na kuwaudhi wengi, ila kwa sababu wauza madawa ndiyo wenye vyombo vya habari, wanampa air time na anadhani anapendwa na wengi kumbe ni sawa na propaganda za ukawa kipindi kile ambapo kwenye kura waliangukia pua pamoja na kuhonga watu hela wapige kura).

Nadhani pia Nape akipata mpinzani jimboni kwake 2020 anaweza asirudi bungeni, maana kutetea wauza madawa imeuzi watu wengi.

Kuhusu Dkt Magufuli kumsifia Nape, hizo ni siasa, lazima atampiga chini siku za usoni.
 
Mkuu wa mkoa na uwazir wa michezo .
Uwazir ni mkubwa but kimajukumu ukuu wa mkoa ni mgumu na muhimu.
Makonda anafaa uwazir wa mambo ya ndan.
 
Back
Top Bottom