Kati ya kilimo na kujenga reli kipi kinaweza kumaliza umasiki kwa haraka

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Kati ya kilimo,na kujenga reli,ni kipi kinaweza kumaliza umasikini kwa haraka?
Kwa maoni yangu tunatatizo mahali flan,hatuna uwezo wa kuchagua ni mambo yapi ni muhimu kwa wakati,hatuna uwezo wa kuchagua ni kipi sahihi,na kwa wakati gani,kupanga ni kuchagua,lkn mm ningelikuwa ni rais,au ningelikuwa ni spika wa bunge ningeakikisha pesa za kujenga reli,na pesa za kununua ndege,nazipeleka kwenye kilimo cha umwagiliaji!! Mfano serekali ingepeleka pesa za ndege,na pesa za reli kwenye kilimo,ninaamini kwenye kilomo kuna lipa zaidi kuliko kwenye kununua ndege,na kujenga reli,lkn ndio hivyo tena serekali,na bunge limeshafikia maamuzi,tusubiri muda uamue
 
Mkuu umebanwa na nini mbona una haraka hivyo..?
Lakini hata hivyo sio Kilimo wala Ujenzi wa Reli kinaweza kukukomboa maana vingi vinakuwa kwenye makaratasi refer "KILIMO KWANZA" watu walienda mpaka Malaysia kujifunza.
Jitihada zako tu mkuu ndio zinaweza kukukomboa, maana Watanzania kwa jinsi tulivyo hayo unayoyasema yakifanyika tutaanza kulalamika Serikali itutafutie Masoko.
 
Kilimo kwanza kilimo kikishamiri hata mfumuko wa bei utapungua hebu fikiria kama tuna network nzuri za barabara mpaka vijijini mtanzania ataweza kula milo mitatu kwa siku vingine ni anasa tu.
 
Ukiishi na mwanadamu asiyelalamika,hawezi kuwa mzima,maiti ndio huwa hazilalamiki
 
Lkn angalao unga ulikuwa na bei nzuri zaidi
 
Yaa una point sehem fulan lakin labda nikuulize hayo mazao yanakua ya kuuza nje au kukidhi upungufu hapa kwetu ili kuweka uwiano mzr sokon?? Maana tukizalisha sana bado itakua salama kwa chakula kwetu swal je kikizid tunafanyaje?au tutarid hapa kulalamika kama walima nyanya wa mwaka jana??

Pili njia kipi ni gharama sana kukitengeneza? Kama ni reli bas tuanze na reli ili baadae tukiweka kwa kilimo hata kubeba kwa uhakika inakua fasta zaid,,

Ila una hoja sema tu unataka kifanyike unachopenda wewe
 
Ukiishi na mwanadamu asiyelalamika,hawezi kuwa mzima,maiti ndio huwa hazilalamiki

Say or speak nothing and do nothing, you're as good as dead!
Dunia imeingia kwenye shida na matatizo kwa vile watu wema waliamua kukaa kimya!!!Lazima watu wema waseme kitu ili mambo yakae sawa!

Baba wa Taifa aliwahi kusema,KUPANGA NI KUCHAGUA. Kama Taifa lazima liwe na DIRA,DHAMIRA YA DHATI NA VIPAUMBELE VYAKE(Priorities)|
Kwasasa Taifa limepoteza mwelekeo, wanasiasa waliogushi vyeti wameteuliwa na kuachwa waongoze ilhali hawana ABC au weledi wowote katika Uchumi,Kilimo na Biashara!
Angalia mfano mdogo huu: KILIMO KWANZA iliishia kwenye makabrasha tu! Mtu anatangaza Kilimo Kwanza lakini Wizara ya Kilimo inatengewa Tshs. 400m za Kilimo kununua Matrekta lakini fedha ya Chai na Vitafunwa ni Tshs. 2 Bilioni!!!!
Leo wanatuambia Nchi ya Viwanda lakini Wizara ya Viwanda haina fedha ya Kujenga Viwanda! Fedha xote zimepelekwa kwenye KUHAMIA DODOMA, KUNUNUA NDEGE,KUJENGA STANDARD GAUGE na upuuzi mwingine wa kukurupuka!
Kwanini usipeleke Fedha kwenye KILIMO na VIWANDA ili Kilimo kizalishe mazao ambayo mwisho wa siku yatapelekwa viwandani kwa ajili ya kuchakatwa ili kuongezewa thamani??
Kutokana na Uzalishaji kwenye Kilimo na Viwanda Serikali itaweza kuuza bidhaa nje baada ya kuongezwa thamani through industries/factories na itapata fedha za kigeni ili kujenga hiyo Reli ya SG na baadaye kununua hizo ndege za Boeing inazo zihangaikia kwa sasa?
Hivi Jacob Zuma angelimwuliza JPM juzi kwamba unaomba nikukopeshe fedha ya kujenga reli ya SG mbona nasikia umenunua Boeing kwa fedha Taslimu au hata kama ni kwa PP? Hapa inaonekana hakuna priority! Maana reli kwa maana ya Treni ina uwezo mkubwa wa kusafirisha Mizigo na Abiria kuliko ndege!
Alichofanya JPM ni ile wazungu wanasema KUWEKA MKOKOTENI MBELE YA FARASI!!!Yaani badala ya Farasi kuvuta mkokoteni unalazimisha mkokoteni ndo uvute farasi!! Nonsense!!!
 
Mi mwana mbagala siwaelewi hadi mniambie TAZARA ilikuwa na tatizo gani. Hii reli bila Bandari ya mkwere ni kazi bure tu. Lakini pia bora hiyo. Ila kwenye ndege, ni kukurupuka kukubwa. Hiyo pesa ingeingizwa kwenye horticulture vijana wangetoka sana, asingebaki mtu hapa mbagala.
 
Kati ya kilimo,na kujenga reli,ni kipi kinaweza kumaliza umasikini kwa haraka?
Kwa maoni yangu tunatatizo mahali flan,hatuna uwezo wa kuchagua ni mambo yapi ni muhimu kwa wakati,hatuna uwezo wa kuchagua ni kipi sahihi,na kwa wakati gani,kupanga ni kuchagua,lkn mm ningelikuwa ni rais,au ningelikuwa ni spika wa bunge ningeakikisha pesa za kujenga reli,na pesa za kununua ndege,nazipeleka kwenye kilimo cha umwagiliaji!! Mfano serekali ingepeleka pesa za ndege,na pesa za reli kwenye kilimo,ninaamini kwenye kilomo kuna lipa zaidi kuliko kwenye kununua ndege,na kujenga reli,lkn ndio hivyo tena serekali,na bunge limeshafikia maamuzi,tusubiri muda uamue
Tuanze miundo mbinu kwanza (reli ,barabara) ili msisitizo wa kilimo unapokuja ,tuwe na urais wa kufikisha product sokoni
 
unapolima lazima uhakikishe kuna soko na kama kuna soko lazima uhakikishe kuna miundo mbinu ya kupeleka mazao shambani kuna sehemu mazao yanaoza sababu hakuna miundi mbinu mizuri ya kupeleka mazao sokoni ni muhimu sana kwa nchi yetu tukiwa na reli tuna uhakika wakulima na wafanyabiashara wataweza kuleta mazao ya kwa uhakika
 
Tulikua na kilimo ni uti wa mgongo tokea enzi za Nyerere,tukaja na kilimo kwanza miaka 8,yote hukuyaona mkuu?
Sasa tunajenga reli ya kisasa.kupanga ni kuchagua
 
tunayo reli inafika mpaka south africa mbona imeshiwa kutukomboa zimeuzwa mpaka kota za wafanyakazi bora kilimo
 
Kati ya kilimo,na kujenga reli,ni kipi kinaweza kumaliza umasikini kwa haraka?
Kwa maoni yangu tunatatizo mahali flan,hatuna uwezo wa kuchagua ni mambo yapi ni muhimu kwa wakati,hatuna uwezo wa kuchagua ni kipi sahihi,na kwa wakati gani,kupanga ni kuchagua,lkn mm ningelikuwa ni rais,au ningelikuwa ni spika wa bunge ningeakikisha pesa za kujenga reli,na pesa za kununua ndege,nazipeleka kwenye kilimo cha umwagiliaji!! Mfano serekali ingepeleka pesa za ndege,na pesa za reli kwenye kilimo,ninaamini kwenye kilomo kuna lipa zaidi kuliko kwenye kununua ndege,na kujenga reli,lkn ndio hivyo tena serekali,na bunge limeshafikia maamuzi,tusubiri muda uamue
Reli itamaliza umaskini haraka kama ikipita Magu.
 
Kila kitu kinataka chenzake kiwepo. Yaan kwenye uchumi huwezi kutegemea sector moja. Mazao yanahitaji soko, yanahitaji kusafirisha ili yaende sokon. Mazao yako ya aina nyingi, mfano nyanya, matunda, mahindi, mpunga au mchele, nk. Kuna mengine yanahitaji usafiri wa haraka ili yafike sokon vinginevyo yanaharibika. Kuna mengine yanahitaji wanunuzi wa hapo hapo so lazima ufanye mpango wa kuleta watalii au wa kujenga viwanda. Viwanda vinahitaji soko. Soko ni watu na watu tunao tatizo ni namna ya kuwafikia watu Kwa haraka. Unahitaji barabara, reli na ndege na Hata meli za uhakika. Madaraja nk.

Sasa ni wewe tu kuamua uanze na kipi ili kuweza kufikia lengo. Ni kupanga kipi kianze na kipi kifuate. Wachumi wamesema kipi ukikifanya kita stimulate chenzake. Yaan kuna vitu ukivifanya vinasababisha vingine vije bila kutumia nguvu kubwa.

Na ndo maana wenye akili tunaona wazi kuwa Kwa speed hii ya Magu, ukimpa miaka kumi na akaendelea na speed hii hii, tutakuwa mbili sana. Baada ya miaka minne kutoka sasa mambo mengi yataanza kutokea tu yenyewe bila kutumia nguvu kubwa.

Sasa Kuja kwenye wazo lako. Ni mawazo ya mtu alie na njaa ambaye anadhani akishashiba inatosha atakuwa hahitaji kitu kingine Chochote cha ziada wakati sio Kweli. Ni mawazo ya kitoto tu.

Wenye akili wanawaza miaka kumi mpaka ishirini ijayo na ndio tofaut yako ww na mzungu au mtu aliefanikiwa. Ww unawaza Leo wenzako wanawaza future itakuwaje. Wanaiona leo. Wana ishape leo.

Ndio tofaut iliyopo Kati yenu nyie na Magu, na hamtamuelewa kabisa. Na hamuwezi kumuelewa Kwa sbb mnawaza leo.

Na ndo maana huna nafas yoyote kubwa ya maamuzi Kwa sabb huwezi kuwaza future ya taasisi unayoiongoza.

Sawa Sawa tu na akina mangungo ambao waliuza nchi wanayoishi Kwa tamaa ya kipande kidogo cha kitambaa bila kuwaza kuwa vipi baada ya kuuza yeye ataishi wapi. Hakuwaza future na wabongo tumerithi akili hizo.
 
Kati ya kilimo,na kujenga reli,ni kipi kinaweza kumaliza umasikini kwa haraka?
Kwa maoni yangu tunatatizo mahali flan,hatuna uwezo wa kuchagua ni mambo yapi ni muhimu kwa wakati,hatuna uwezo wa kuchagua ni kipi sahihi,na kwa wakati gani,kupanga ni kuchagua,lkn mm ningelikuwa ni rais,au ningelikuwa ni spika wa bunge ningeakikisha pesa za kujenga reli,na pesa za kununua ndege,nazipeleka kwenye kilimo cha umwagiliaji!! Mfano serekali ingepeleka pesa za ndege,na pesa za reli kwenye kilimo,ninaamini kwenye kilomo kuna lipa zaidi kuliko kwenye kununua ndege,na kujenga reli,lkn ndio hivyo tena serekali,na bunge limeshafikia maamuzi,tusubiri muda uamue
Amini usiamini reli na barabara vitatukomboa

Amini usiamini Mkuu reli na barabara vitatukomboa in the near future. Hasa Kwa kuwa access to market ni tatizo Kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom