Kati ya CCM na CHADEMA nani alishirikiana na wezi wa rasilimali zetu?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,441
Wasalaam wana JF
Swali hapo juu lahusika

Nimeona katika Bunge wanawashambulia wabunge wa CHADEMA kama Lisu na Mnyika eti ni wezi wanashirikiana na wawekezaji wa madini hasa kampuni ya ACACIA kutuibia madini yetu na hii baada ya Rais pombe kuzuia mchanga wa madini

Kimsingi hasara yote wizi wote tunaofanyiwa Watanzania kuhusu rasilimali zetu ni uzao wa CCM yani CCM ndo chanzo cha umaskini wa Watanzania juzi gazeti la Mwananchi limeandika namna rasilimali zetu zisivyotunufaisha Watanzania na serikali na hii yote ni kutokana na serikali ya CCM na wabunge wao kukaa na kupitisha sheria mbovu ambazo leo wanageuka na kuwaonea wabunge wa upinzani ambao kimsingi miaka mingi

Waliipinga hii mikataba mibovu.CCM acheni kujitekenya wenyewe lazima mjue nyie ndo chanzo cha matatizo yote kwenye nchi hii,huyo anaezuia Makinikia nae alikuwepo kwenye Baraza la mawaziri anajua ulaghai waliotufanyia Watanzania Leo hii mnawashutumu

Wabunge wa upinzani utadhani wao ndo walishika Dola kipindi inasahiniwa hiyo mikataba mibovu ya kinyonyaji.
AIBU KWA CCM
 
Kule bungeni maccm yanazinduka kutoka usingizini na kusema ndiyo mwisho wa siku tunalaumu vichwa kama akina lisu kwa kuyanawisha uso haya maukoo ya panya.
 
CCM ni kama ukoo wa panya.Baba mwizi,mama mwizi.Babu na bibi wote wezi-Joshua Nasari
 
Wasalaam wana JF
Swali hapo juu lahusika
Nimeona katika Bunge wanawashambulia wabunge wa CHADEMA kama Lisu na Mnyika eti ni wezi wanashirikiana na wawekezaji wa madini hasa kampuni ya ACACIA kutuibia madini yetu na hii baada ya Rais pombe kuzuia mchanga wa madini

Kimsingi hasara yote wizi wote tunaofanyiwa Watanzania kuhusu rasilimali zetu ni uzao wa CCM yani CCM ndo chanzo cha umaskini wa Watanzania juzi gazeti la Mwananchi limeandika namna rasilimali zetu zisivyotunufaisha Watanzania na serikali na hii yote ni kutokana na serikali ya CCM na wabunge wao kukaa na kupitisha sheria mbovu ambazo leo wanageuka na kuwaonea wabunge wa upinzani ambao kimsingi miaka mingi waliipinga hii mikataba mibovu.CCM acheni kujitekenya wenyewe lazima mjue nyie ndo chanzo cha matatizo yote kwenye nchi hii,huyo anaezuia Makinikia nae alikuwepo kwenye Baraza la mawaziri anajua ulaghai waliotufanyia Watanzania Leo hii mnawashutumu wabunge wa upinzani utadhani wao ndo walishika Dola kipindi inasahiniwa hiyo mikataba mibovu ya kinyonyaji,

AIBU KWA CCM
Ni kweli mkuu mh Tundu. Lakini naomba unijibu hili swali langu.

Ni uzembe kuacha mlango wazi kisha mwizi akaingia ndani ya nyumba na kuniibia mali yangu. Hiyo nakubaliana nayo kwa 100%

Sasa huyo mwizi aliyeniibia pa1 na kwamba nilikuwa mzembe nimemgundua na anayo mali yangu aliyoniibia. Nataka kumkamata mwizi huyo wewe unamwambia kimbia uifiche hiyo mali kwani mwenye mali kakugundua.

Na nzuri/mbaya zaidi ww unaemwambia mwizi akimbie na kuficha mali yangu aliyoniibia ni mdogo wangu tena tumbo moja. Je mbaya kwa wakati huu wa kupatikana kwa mali yangu ni nani mm niliyeacha mlango wazi na nikaibiwa au wewe unaechangia kupotea kwa mali yangu. Mali ambayo kwa namna moja au nyingine hata wewe ni mali yako.

TANZANIA KWANZA VYAMA BAADAE.
 
wasumu Ndugu yangu siasa sio uadui hayo majina ya ajabu ajabu sio mazur mkuu wangu changia kama mimi nilivyofanya sawa
 
Ni kweli mkuu mh Tundu. Lakini naomba unijibu hili swali langu.

Ni uzembe kuacha mlango wazi kisha mwizi akaingia ndani ya nyumba na kuniibia mali yangu. Hiyo nakubaliana nayo kwa 100%

Sasa huyo mwizi aliyeniibia pa1 na kwamba nilikuwa mzembe nimemgundua na anayo mali yangu aliyoniibia. Nataka kumkamata mwizi huyo wewe unamwambia kimbia uifiche hiyo mali kwani mwenye mali kakugundua. Na nzuri/mbaya zaidi ww unaemwambia mwizi akimbie na kuficha mali yangu aliyoniibia ni mdogo wangu tena tumbo moja. Je mbaya kwa wakati huu wa kupatikana kwa mali yangu ni nani mm niliyeacha mlango wazi na nikaibiwa au wewe unaechangia kupotea kwa mali yangu. Mali ambayo kwa namna moja au nyingine hata wewe ni mali yako.

TANZANIA KWANZA VYAMA BAADAE.


Tatizo ni kuwa unaamini ama unafanana akili au umemzidi akili mwizi huyo kiasi cha kuamini mdogo wako anamfundisha mwizi jinsi ya kukukwepa. Ukweli ni kuwa kiwango cha akili uliyonayo leo, mwizi alikuwanacho kipindi anapanga kukuibia hivyo akapanga atakavyokutoroka hata ikitokea kuwa umemshika na ushahidi mkononi. Sasa jaribu kupiga hesabu ya muda tangu alipoingia hadi sasa na ukadirie kiwango cha elimu ya mwizi.

Mdogo kwako amekupa mbinu ya kupambana na mwizi wako (ambaye kiuhalisia ni mwizi wenu), wewe badala ya kuitumia ili ufanikiwe kuipata mali yako wewe unaanza kukwaruzana naye. Sitaki kuamini kuwa eti mdogo wako ana akili kiasi cha kumfundisha mwizi wako.

Huu si wakati wa kuwaza kuwa nani atapata sifa maana huo ni mtazamo wa kisiasa na hili ni suala la kujenga nchi yetu kwa ajili ya vizazi vinavyofuata. Tumeiharibu na sasa tutulize akili tuirekebishe.
 
Back
Top Bottom