KATAVI: Watu watatu mbaroni kwa kukutwa wakitoa fedha kwenye ATM wakiwa na kadi 19

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
1.jpg

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .

Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea, wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.

Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea fedha .

Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha.

Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha fedha taslimu shilingi 3,680,000.

Amezitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237, AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.

Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC 70408100131.

Amesema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .

Kaimu kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia kwenye ATM za benki.
 
Kama mshahara wa Serikali umetoka,hii huwa inatokezea sana kwa walimu maeneo ya nje ya mji.
Mwisho wa mwezi wanatumana ili kuchukuliana pesa ili kubana matumizi ya pesa ya nauli.

Umenikumbusha mbali sana kuhusu hii ajira ya ualimu vijijini. Binamu yangu alikuwa mwalimu, mwisho wa mwezi anakwambia unaanza kungoja lori linalokuja kuchuka mkaa kijijini, ukifika mjini kabla hujaenda ofisini inabidi utafute mahali uoge, utoe nguo safi kabla hujaenda ofisi ya elimu au bank.
 
Askari viherehere hao na kutafuta Kiki tu! hafu wanawaonea sana wanavijiji wakienda kuchukua pesa zao benki kwenye hizo benk za nmb zilizopo kila wilaya. yani askari wa tz hovyo kabisa yani hawaamini kama kunawafanyakazi wengine wa umma nchi hii isipokua wao tu sijui ndivyo wanavyofundishwa huko moshi au mi siwaelewagi ani. utakuta unamwelesha bana mm ni mtumishi mwenzio idara furani lakini wapi ss ngoja wao wakukute kwenye goli we wanatia huruma hao mpaka basiiii mi huwa nawawekea tint tu.
 
Labda ntakuelewa baadaye! Sijakupuuza najaribu kukuelewa!!!
 
Kuna vile vikampuni vinakopesha kwa riba kubwa na watumishi wanaacha ATM card.
Mwisho wa mwezi wanatoa hela,wanakupa balance yako na ATM card.
Moja ya hayo makampuni ni Amacha credit.
Nina uhakika 99% watu waliokamatwa ni kutoka kwenye hizo kampuni
 
Askari viherehere hao na kutafuta Kiki tu! hafu wanawaonea sana wanavijiji wakienda kuchukua pesa zao benki kwenye hizo benk za nmb zilizopo kila wilaya. yani askari wa tz hovyo kabisa yani hawaamini kama kunawafanyakazi wengine wa umma nchi hii isipokua wao tu sijui ndivyo wanavyofundishwa huko moshi au mi siwaelewagi ani. utakuta unamwelesha bana mm ni mtumishi mwenzio idara furani lakini wapi ss ngoja wao wakukute kwenye goli we wanatia huruma hao mpaka basiiii mi huwa nawawekea tint tu.
We mbona wa hovyo sana! Yaani badala ya kuwapongeza askari kwa kazi nzuri unabwata hovyo! We unadhani kadi hizo wangekuwa wamepewa na kutumwa na wenyewe wangekamatwa hadi sasa? Uwe unabakiza basi hata akili za kuvalia nguo za ndani.
 
Askari viherehere hao na kutafuta Kiki tu! hafu wanawaonea sana wanavijiji wakienda kuchukua pesa zao benki kwenye hizo benk za nmb zilizopo kila wilaya. yani askari wa tz hovyo kabisa yani hawaamini kama kunawafanyakazi wengine wa umma nchi hii isipokua wao tu sijui ndivyo wanavyofundishwa huko moshi au mi siwaelewagi ani. utakuta unamwelesha bana mm ni mtumishi mwenzio idara furani lakini wapi ss ngoja wao wakukute kwenye goli we wanatia huruma hao mpaka basiiii mi huwa nawawekea tint tu.
Una maana askari anakuwa kiherehere kwa kumata wezi? Mbona sikuelewi kabisa? Au unataka askari akimkamata mfanyakazi wa serikali anayefanya uhalifu amwache? Ebu jieleze zaidi. Sijakupata bado.
 
Askari anapokutilia shaka anatakiwa akukamate upelekwe, kituoni utoe maelezo, kama yakijitosheleza uachiwe, ukijikanyaga upelekwe mahamani! Sasa ajabu nn!
 
View attachment 351606

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .

Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea, wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.

Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea fedha .

Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha.

Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha fedha taslimu shilingi 3,680,000.

Amezitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237, AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.

Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC 70408100131.

Amesema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .

Kaimu kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia kwenye ATM za benki.
Hivi pata picha mfano kadi yako imetajwa hapo na upo mkoa wa mbali na account ina zaid ya m10 za mkopo hujazitumia utakua hali gani
 
Ni haki kabisa kwa askari kuwakakamta. Kama wametumwa na wenzao ama vinginevyo wakajieleze huko na hawataonewa kama ni kweli kulikuwa na ulazima wa wao kufanya.hivyo.
Hili jambo la kukopeshwa halafu unampa mkopeshaji kadi ya ATM kila mwisho wa mwezi lilivuma sana na nadhani linaweza.kuwa pia limehusika hapa. Hii tabia inabidi ikomeshwe watu watafute namna nyingine kwakuwa linaruhusu matumizi yasio sahihi ya ATM kadi.
Yote kwa yote naunga mkono.askari kuwakamata.
 
Maeneo mengi nchini walimu wanakopeshwa fedha na wafanyabiashara kwa makubaliano ya kukabidhi ATM card na password kwa mkopeshaji na mshahara unapotoka aliyekopesha ndiyo anakwenda kuchukua fedha kisha anakata yake na kinachobakia ndiyo anampelekea mwenye akaunti (mkopaji). Ni hali ya udhalilishaji sana lakini walimu wengi huko vijijini ndiyo wanavyoishi. Nililiona hili wilayani Kasulu wakati flani nikiwa katika ziara ya kikazi.
 
Back
Top Bottom