Katavi: Watu 5 wamejeruhiwa kwa risasi

Katavi: Watu 5 wamejeruhiwa kwa risasi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,197
Reaction score
64,643
NSIMBO: Watu watano wamejeruhiwa kwa risasi katika kijiji cha kashelami halmashauri ya wilaya ya nsimbo mkoani katavi

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa mapori ya akiba (TFS) kutaka kufyeka mazao katika mashamba ya wakazi wa kijiji hicho yanayodaiwa kuwa ndani yam situ wa akiba

Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Josephat Patrick (27), Godfrey Patrick (34), Filbert Patrick (40) January Patrick (22) na Nkuba Sai (28)

Wakizungumza kwa taabu katika hospitali ya rufaa mjini Mpanda walikofikishwa kwa ajili ya matibabu majeruhi wamesema mara baada ya watu hao kufika walijaribu kuwazuia kufyeka ,Mazao yao ndipo walipoanza kuwafyatulia risasi

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Damas Nyanda amesema jeshi la polisi linafuatilia kwa kina tukio hilo kubaini hasa ni kina nani wametekeleza na shambulio hilo.
 
Washaambiwa waue,,huko katavi si Kwa mzee wa nyuki au
 
Kuna kipindi mtu unapita unajidai hukusoma.....ila moyoni unaumia sana!

Inakuwawaje mnamlima mtu masasi wakati hajatenda uhalifu wa kumlima masasi?

Anyway. Nifunge domo langu!
 
Ndugu wanne wa familia moja katika Kijiji cha Ikongwe, Kata ya Sitalike wilayani Mpanda, wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Katavi, baada ya kudaiwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao na askari wa Wakala wa Hifadhi wa Misitu (TFS) wa Halmashauri ya Nsimbo.

Diwani wa Kata ya Sitalike, Adamu Cherehani jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa sita mchana na kuzua hataruki kubwa kutoka kwa wananchi.

Aliwataja wanakijiji waliopigwa risasi kuwa ni Josephat Patrick (27) aliyepigwa risasi mbili kifuani, Jofrey Patrick (39),aliyejuruhiwa mkono wa kushoto,Fiberiti Patrick (40), alijeruhiwa mguu wa kushoto, Januari Patrick (22), alipigwa risasi ya bega la kulia na mwingine aliyetambulika kwa jina la Nkuba Sai aliyepigwa risasi mkono wa kushoto .

Diwani Cherehani, alidai chanzo cha wanakijiji hao kushambuliwa kwa risasi ni askari wa TFS waliofika kijijini na kuanza kufyeka mahindi yao kwenye mashamba kwa kile walichodai yamelimwa ndani ya eneo la hifadhi ya Msitu wa Msaginya .

Baada ya kupata taarifa mahindi yao yanafyekwa, wanakijiji hao waliokuwa zaidi ya kumi walifika mashambani na kuwasihi askari hao waache kufyeka mazao yao kwa sababu ndiyo wanategemea kwa chakula na familia zao, lakini waliwagomea.

Alisema askari waliendelea kufyeka mahindi hayo, hali ambayo iliwafanya wanakijiji waanze kuwazomea.

“Haya mahindi yalikuwa yamebakiza mwezi mmoja tu yaive, lakini askari wamefyeka yote, jambo hili linatia uchungu,”alisema.

Kutokana na hali hiyo, wananchi walianza kuwazomea askari hao wakati wanaingia kwenye gari lao aina ya Toyota LandCruser, ghafla wakaanza kurusha risasi ovyo.

Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo (CCM) alisema amesikitishwa na kitendo hicho kwani hawakuwa na sababu ya kutumia nguvu kubwa kiasi hicho kuwakabili wananchi ambao hawakuwa na silaha.

Alisema eneo hilo linalodaiwa mali ya TFS, lilipimwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2002 na kutenganisha maeneo ya hifadhi na shughuli za binadamu

Alisema eneo hilo lilipimwa tena mwaka huu chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kabla ya kuanzishwa Halmashauri ya Nsimbo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hatua zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Alisema alikwenda eneo hilo la tukio kuokota ganda moja la risasi ambayo inaonekana kuwa ni gobore.

Alisema ameagiza kukamatwa mara moja kwa askari wa TFS waliohusika kufanya kitendo hicho ili waweze kuhojiwa na sheria kuchukua mkondo wake wake.
 
Achana nao ... hao wote walimpigia jiwe kura .. so wameanza kuvuna mazao ya walicho kipanda ..

Kiubinaadamu inauma kuona binaadamu mwenzako anafanyiwa hujuma/unyama .. lakini sasa kama aliamua mwenyewe kulichuma janga hauwezi kumzuia asile na wakwao ..

Hapo ndio wajue sasa kwamba tz ..Nyati .simba .sokwe na wanyama pori wote wana thamani kuliko utu wao ...
 
Ndiyo kosa la kuchukua watu waliofeli mitihani na kuwapa silaha za moto. Wengi wao wanatumia nguvu kuliko akili za kawaida.

[emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22] Huyo askari ajaribu kuvaa viatu vya hiyo familia, angekuwa katendewa yeye unyama huo angekuwa na imani na polisi au vyombo vya usalama tena?
 
Eti eneo la tukio liliokotwa ganda moja la rossi ya gobore.Ukanjanja wa hali ya juu maana gobore halina ganda la risasi
 
Afu sisi ambao tulishupaza mishipa ya shingo kuwasihi waachane na ccm kwani imejaa dhuluma hata majanga kama hayo hayawezi kutukuta kwani tunakula kwa kalamu zetu.
OK haina shida tutaenda tena 2020 kuwakumbusha tena.
 
Kuna kipindi mtu unapita unajidai hukusoma.....ila moyoni unaumia sana!

Inakuwawaje mnamlima mtu masasi wakati hajatenda uhalifu wa kumlima masasi?

Anyway. Nifunge domo langu!
Ni tamaa tu za kulima batu masasi maana wana masasi lakini hakuna vita kabambe juu ya nini wasilime bamutu masasi?
 
Kuna kipindi mtu unapita unajidai hukusoma.....ila moyoni unaumia sana!

Inakuwawaje mnamlima mtu masasi wakati hajatenda uhalifu wa kumlima masasi?

Anyway. Nifunge domo langu!
Huko Katavi hali ya uharibifu wa misitu, Unaofanywa na wahamiaji wasukuma ni mbaya sana.... Watu hawa wakiachwa hata miaka miwili tuu walahi utakuta jangwa. Huko kwao wanakotoka wameharibu everything na sasa wanakimbilia huko Katavi na Kigoma Kwa maelfu.
 
Huko Katavi hali ya uharibifu wa misitu, Unaofanywa na wahamiaji wasukuma ni mbaya sana.... Watu hawa wakiachwa hata miaka miwili tuu walahi utakuta jangwa. Huko kwao wanakotoka wameharibu everything na sasa wanakimbilia huko Katavi na Kigoma Kwa maelfu.
Ndio umuue kwa risasi kwa sababu tu ameingiza mifugo kwenye eneo tengwa?

Huu uhalali wa kumuua mtu huyu unayemuita msukuma kwa kwa kuharibu mazingira kwa kulisha mifugo eneo linalokazwa mnaupata wapi?

Nani anawalisha uongo kwamba kwa namna tunavyoishi tunaleta eneo kuwa jangwa kuliko wazalishaji wa hewa ya ukaa USA na Uchina?

Kwamba wasukuma hao wanasababisha eneo kuwa jangwa kuliko ujenzi wa stigla?

Kuweni na huruma na watu. Hawa nao ni watu kama wewe na nduguzo.

Leo unasema eti wametoka huko kwao, wewe ulipo hapo ni kwenu?


Ujinga ujinga ujinga tu!
 
Nadhani kwa matendo tunayotendewa watanzania kwa sasa, kwa vyovyote Mungu atakuwa ametuacha! Haiwezekani John aue watu na kufurahia kama alivyokuwa anafanya farao halafu hata viongozi wa kiroho nao wafurahie pia!
Turudini kwenye toba tumuombe Mungu atuondolee adhabu hii ya umauti kwakweli.
 
Back
Top Bottom