figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,715
- 59,249
Wakazi wa Mtaa wa Kigamboni Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameeleza kukasirishwa na kitendo cha askari mmoja wa kituo cha Polisi Mpanda Mjini kuwaita wananchi wa mtaa huo kuwa ni Kenge akiambatanisha na matusi mengine ya aibu.
Wakazi hao, wamedai kesho watafanya maandamano ya amani kuelekea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, pamoja na mambo mengine, watakuwa wakipinga kitendo cha Jeshi la Polisi kumwachia ALLY BWANA au KARIM RAMADHANI anayetuhumiwa kuwapiga wananchi na wengine kuwasababishia ulemavu.
=====
MPANDA Wakazi wa Mtaa wa Kigamboni Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameeleza kukasirishwa na kitendo cha askari mmoja wa kituo cha Polisi Mpanda Mjini kuwaita wananchi wa mtaa huo kuwa ni Kenge akiambatanisha na matusi mengine ya aibu.
Wakazi hao wameeleza kukasirishwa na kauli ya polisi huyo wakati wa tukio la maandamano ambayo yamefanyika mtaani hapo wakishinikiza mkazi mmoja anayefahamika kwa majina ya Ally Bwana au Karim Ramadhani aondoke haraka katika mtaa huo kwa madai kuwa wananchi wengi amekuwa akiwapiga na kuwasababishia ulemavu.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigamboni Joseph Kambaulaya amekiri kupokea malalamko dhidi ya Ally Bwana ambaye amekuwa kero ambapo amesema jeshi la polisi liendelee kumshikilia mtu huyo kwani kitendo cha kumwachia arudi mtaa wa Kigambano kunaweza kusababisha wananchi kujichukulia sheria mikononi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Bededicti Mapugila amesema mpaka sasa hajapata taarifa kuhusu tukio hilo ambapo kwa mjibu wa mwenyekiti wa mtaa Joseph Kambaulaya Ally Bwana amekamatwa mara tatu na kuachiwa kisha kuendelea kujigamba kuwa Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Mpanda yuko chini yake ndiyo maana hawezi akafungwa. Mtaa wa Kigamboni una zaidi ya kaya 15000 sawa na wakazi 5000.