Katavi: Mwalimu auawa baada ya kukataa kununua Pombe

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani kata ya Kakese, Shauri Kiani (35) amefariki baada ya kupigwa na tofali kichwa kutokana na kukataa kumnunulia pombe anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Leo Ijumaa Machi 6, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea tukio, “limetokea Machi 3, 2020 saa 5 usiku eneo la Mbugani.

Mtuhumiwa ni Omary Juma (30) mkazi wa Kakese. Kiani alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi lakini alifariki wakati anapatiwa matibabu.”

Amesema polisi walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa anayeendelea kuhojiwa, kwamba muda wowote atafikishwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom