KATAVI: Mchungaji akamatwa na Meno 11 ya Tembo akiwa 'ameyahifadhi' kanisani

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,670
Imeandikwa na Walter Mguluchuma | Katavi yetu Blog | Mei 09, 2016


Jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa kushirikiana na Askari wa TANAPA wa Hifadhi ya wanyama ya Katavi wamemkamata mchungaji wa Kanisa la Moroviani Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele akiwa na mtu mmoja ambao wajina yao yamehifadhiwa wakiwa na meno ya tembo 11 yenye thamani ya shilingi milioni 90 wakiwa wameyahifadhi ndani ya Kanisa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia waandishi wa Habari jana ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa mbili na nusu katika Kanisa la Moroviani ililoko katika Kijiji cha Usevya.

Alisema Mchungaji huyo wa Kanisa la Moroviani akiwa na mwenzake mmoja ambao majina yao yamehifadhi kwa sababu za kiupelelezi walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia Jeshi la Polisi na kwa Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa watu hao wanajihisisha na biashara hara haramu ya meno ya Tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya Kanisa.

Baada ya taarifa hizo polisi na Tanapa walianza kufanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo walizozita kutoka kwa Raia wema hukusiana na tuhuma za biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo.

Kaimu Kamanda Nyanda alieleza ndipo jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Tanapa walipoweza kufika katika Kanisa la Moroviani Usevya na kufanya upekuzi ndani ya Kanisa hilo.

Katika upekuzi huo waliweza kukamata meno ya Tembo vipande 11 yenye uzito wa kilogramu 20.3 yenyethamani ya shilingi Milioni 90 yakiwa yamehifadhiwa ndani ya tenga la kubebea mizigo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya Kanisa la Moroviani Usevya lililokuwa likiongozwa na mchungaji huyo anaeshikiliwa na Polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliotokea Mei 8 majira ya saa mbili usiku huko Katika maeneo ya Mgolokani Kata ya Sitarike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Katavi walimkamata mtu mmoja ambae jina lake limehifadhiwa akiwa na jino moja la Tembo ..

Kwa mujibu wa Nyanda mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya Askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake mtuhumiwa na ndipo walipo weza kukamatwa na jino moja la Tembo likiwa limefifadhiwa ndani ya nyumba yake .

Tukio la pili lilitokea siku hiyo hiyo katika maeneo ya Mgolokani Kata ya Sitalike ambapo mtu mmoja ambae nae jina lake limehifadhiwa kwa ajiri ya upelelezi alikamatwa akiwa na jino moja la Simba akiwa amerihifadhi ndani ya nyumba yake.

Mtuhumiwa alikamatwa baada ya kufanyika upekuzi ndani ya nyumba yeke na ndipo alipokamatwa akiwa na jino moja la samba akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake

Kaimu Kamanda Damas Nyanda alisema watuhumiwa wote waliokamatwa kwenye matukio hayo matatu wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinawazowakabili.

Ametoa wito kwa wananchi wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama vile uharibifu wa rasilimali za Taifa mfano vitendo vya ujangili uwindaji haramu kuacha mara moja na badala yake wafanya shughuli harali katika kujipatia kipato chao.
 
Tena wahakikishe huyo mchungaji anafungwa kifungo cha maisha kwani atakuwa amewakwaza waumini wengi. Mimi ni mkristo lakini mambo ya kusema eti sijui huyo ni mwenzetu, anaonewa na mfumo hauna nafasi. Funga kabisa huyo mchungaji ikibidi na hilo kanisa piga kitanzi kabisa kama nalo lilijua jambo hilo likakalia kimya uhuni huo.

CC: Ritz, the big show, faizafoxy
 
Mchungaji ndio cheo chake, ila ni binadamu ambaye hupatwa na vishawishi na asikokujua imara katika kusali, atabaki kuitwa mchungaji tu na mbinguni haendi. Kwahiyo wala usiumize kichwa ni kawaida.
 
Sijui nimwamini nani tena.

Mimi nilishakata shauri siku nyingi Mkuu. Naamini kama Kweli Mungu yupo lakini nina mashaka makubwa na Mungu tunayeaminishwa makanisani. Uwe na imani kuwa yupo (the Supreme God to whom all souls belong). na kufanya matendo mema. Lakini kwenda Makanisani na misikitini!! utakatishwa tamaa tu na kubaki kwenye dilemma.

Wale wanaosema wanamtumikia na kumtangaza Mungu, matendo yao ndo hivyo tena.
 
Wamtoze faini ya bilion 135 kama wale wachina au miaka 25 jela. ~skamoo pesa~
 
Sikiliza na ufuate mafunzo yake na usifuate matendo yake kabisa .. Kwani naye hukumu yamsubiri kama sisi ..
 
Back
Top Bottom