Katavi: Mahakama yamhukumu kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, imemhukumu Lazaro Ngomalala (50), mkazi wa Kijiji cha Sibwesa wilaya ya Tanganyika kifungo cha maisha baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa, alisema mahakama imeridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka uliotolewa mahakamani hapo, ukiwamo wa mwanafunzi aliyebakwa.

Kabla ya kutoa hukumu, Ntengwa alisema mtu yeyote anayefanya kitendo kama alichofanyiwa mtoto huyo, anakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili na kifungu cha sheria namba 131, kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu.

Alieleza kutokana na ushahidi uliotolewa , ukiwamo wa mtoto mwenyewe aliyebakwa na mwenzake ambaye alishuhudia tukio hilo, mahakama pasipo kuacha shaka yoyote, imemkuta na hatia mshtakiwa Ngomalala.

Hakimu Ntengwa alisema miongoni mwa ushahidi uliosababisha mahakama imtie mshustumiwa hatiani ni ule uliotolewa na mtoto aliyebakwa na mwenzake mwenye umri wa miaka saba , alisema licha ya kuwa na umri mdogo, watoto hao walitoa ushahidi kwa ufasaha mkubwa dhidi ya tukio hilo.

Pia alisema mahakama ilijiridhisha na ushahidi uliotolewa na muuguzi wa zahanati ya Sibwesa, aliyemfanyia uchunguzi na kubaini mtoto huyo alikuwa amebakwa, hali iliyomlazimu amwanzishie dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Kabla ya kusoma hukumu, Hakimu alitoa nafasi kwa mtuhumiwa kama ana sababu ya msingi ya kujitetea ili aishawishi mahakama impunguzie adhabu.

Katika kujitetea kwake, aliiomba mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa yeye hakutenda kosa hilo bali amesingiziwa na mama mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimdai fedha alizomkopesha.

Hata hivyo, Hakimu Ntengwa alisema kutokana na mshitakiwa kupatikana na hatia, mahakama inamhukumu mshtakiwa kifungo cha maisha jela.

Awali, Wakili wa Serikali Fravian Shiyo, alidai mahakamani hapo kuwa Lazaro alitenda kosa hilo Oktoba 12, mwaka jana, majira ya saa nne asubuhi kijijini hapo.

Ilidaiwa kuwa siku ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto aliyemtendea kitendo hicho akiwa na mtoto mwenzake wakiwa wanacheza jirani na nyumba yao ndipo alipowadanganya wamfuate nyumbani kwake ili akawape fedha wakanunue biskuti na soda.

Shiyo alidai kuwa wakati wakiwa wanakwenda nyumbani kwa mshitakiwa, walipofika kwenye eneo la tangi la maji, Lazaro alianza kumbaka na mtoto huyo kuanza kupiga kelele, lakini hakumwachia mpaka alipo maliza aja yake.


Chanzo: Muungwana Blog
 
Vizuri kama kweli alibaka basi anastahili adhabu.

Siku zote sheria ipo kwa ajili kuwafunga maskini.
 
Siku zote masikini ndio hukutwa na hatia.

Kuna yule kigogo aliyemuua dereva wa daladala kweupe enzi za JK hakukutwa na hatia.
 
Siku zote masikini ndio hukutwa na hatia.

Kuna yule kigogo aliyemuua dereva wa daladala kweupe enzi za JK hakukutwa na hatia.
Acha uongo,Ditto alishtakiwa Kwa kufua Bila kukusudia akapata shaman,bahati mbaya alikufa Kabaka kesho haijaisha.
 
Siku zote masikini ndio hukutwa na hatia.

Kuna yule kigogo aliyemuua dereva wa daladala kweupe enzi za JK hakukutwa na hatia.
Wenye akili walipitia mlango wa nyuma.

"Baada ya kuona kosa ni kuua bila kukusudia" Mkipindisha wenye weledi wanatenda vingine.
 
Back
Top Bottom