figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,191
- 64,607
HALMASHAURI ya Wilaya ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, imeshauriwa kuanzisha bucha maalumu kwa ajili ya kuuza nyama ya kiboko ikiwa ni mkakati wa kuwapunguza viboko waliopo katika bwawa la Milala ambao wamekuwa ni tishio kwa maisha ya wananchi.
Ushauri huo ulitolewa jana na Mhifadhi wa Ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Francis Kona, kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya ya Mpanda (DCC), kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo.
Awali kabla ya kutoa ushauri huo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo Meya wa Manispaa hiyo, Willy Mbogo, waliiomba Wizara ya Maliasili na Utalii, kuwaondoa viboko walioongezeka kwenye Bwawa la Milala ambao wamekuwa wakiwashambulia wakazi wa mji huo na kuwahamishia kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Walidai kuwa tatizo la viboko wanaoishi kwenye Bwawa la Milala ambalo ni maalumu kwa ajili ya maji ya matumizi ya wakazi wa manispaa hiyo, wamekuwa wakiwashambulia wananchi na kuwajeruhi na kufanya uharibifu wa mazao pindi wanapokuwa wametoka kwenye maji na kwenda nchi kavu. Meya huyo alisema suala hilo limeshatolewa taarifa kwa viongozi wa mkoa na Wizara ya Maliasili na Utalii lakini hadi sasa hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa.