Kasulu: UKAWA yaipasua kichwa CCM

Kasulu: UKAWA yaipasua kichwa CCM

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
192
Reaction score
23
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umekuwa tatizo kuu linalo isumbua CCM kiasi cha kuanza mikakati kudhoofisha jitihada zinazofanywa na umoja huu kivyovyote vile hata kwa kufanya makosa ya jinai, imefahamika mjini hapa. Hii imetokana na ukweli kuwa umoja huo umeonyesha taa ya kijani kwa mafanikio ya kuiondoa CCM madarakani, hivyo kila upande unaoonekana kuhusika na UKAWA kufanyiwa kila aina ya hila. Jinai hizo ni pamoja na kushusha bendera za CHADEMA na NCCR MAGEUZI na kuzichoma moto.

Hali imezidi kuwa mbaya zaidi hapa Kasulu Mjini juzi baada ya kuwasili kwa Mh. Moses Machali ambaye ni Mbunge wa Jimbo hili la Kasulu Mjini, NCCR MAGEUZI akitokea Bungeni Dodoma ambapo alikuwa akihudhuria kuwawakilisha wananchi wa Kasulu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh. Moses Machali mbali na kuwa Mbunge pia ni waziri kivuli wizara ya UCHUKUZI akiwakilisha kambi rasmi ya upinzani bungeni, na pia ni Naibu Katibu Mkuu NCCR MAGEUZI TAIFA chama ambacho ni wadau wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Hii imemuongezea maadui mamluki wanaopandikizwa na CCM ili kudhoofisha jitihada zake za mapambano dhidi ya serikali dhalimu ya CCM. Muda mfupi kuanzia sasa ikifika saa 9:00 alasiri atakuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kasulu Mjini katika ukumbi wa COmmunity Centre. Kuna tetesi kuwa agenda kuu ni SERIKALI YA CCM HAITAKIWI IONDOLEWE MADARAKANI, SERIKALI TATU HAZIEPUKIKI, na WAJIBU NA UMUHIMU WA WAFANYABIASHARA KWA MAENDELEO YA KASULU NA TAIFA KWA UJUMLA.

Ujio huu wa Moses Machali umekumbwa na changamoto ya mamluki kushusha bendera iliyokuwa Stand ya Taxi Kasulu Mjini jana jioni. Hivi karibuni ilishushwa ya CHADEMA iliyokuwa Standi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani shughuli ambayo inaratibiwa na UVCCM Kasulu na kutekelezwa na baadhi ya vijana wa kijiwe cha waendesha bodaboda Stand Kuu ya Taxi Kasulu Mjini. Ninawasikitikia ukiwaangalia ni wasakatonge, mguu nje mguu ndani watakuja kujuta kushusha bendera hizo ambazo walizichoma moto.

Hali hiyo inasababishwa na ukweli kwamba hapa Mjini Kasulu hakuna vyama pinzani pasua kichwa kwa CCM kama CHADEMA na NCCR MAGEUZI, hivyo basi kwa kuwa kinafasi ya ubunge Moses anaonekana kuwa ndiye ana nafasi kubwa mpaka sasa ya kurudi Bungeni 2015 wanaendesha hila hizo kukwamisha jitihada za muungano wa UKAWA ukizingatia CCM wanawasiwasi ikiwa UKAWA watasimamisha mgombea ubunge mmoja na kumuunga mkono, Kasulu mjini lazima atakuwa Mh.Moses Machali. Hii inawapasua kichwa CCM hawalali. Mbali na kikao hicho cha ndani Jumamosi tarehe 05/07/2014 atakuwa na mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya stand ya taxi Kasulu Mjini.

VIVA UKAWA, VIVA MACHALI ALUTA CONTINUA.
 
Kulikuwa na taarifa hapa jana kuwa ofisi ya chadema kasulu pamoja na samani zake imetaifishwa baada ya kushindwa kulipa fedha ya pango.ngoja niitafute niiweke hapa
 
Hatuiitaji toa hoja zinazomuhusu mh. Machali acha porojo we msaka tonge
 
CHADEMA yashindwa kulipia pango ya ofisi Kasulu
Ofisi ya Chama cha demokrasia na maendeleo jimbo la kasulu mjini inashikiliwa na mwenye nyumba kwa miezi kadhaa hivi sasa baada ya chama hicho kushindwa kulipa kodi ya pango.

Akiongea kwa masikitiko makubwa mmiliki wa jengo hilo (jina limehifadhiwa) ameeleza kuwa hadi mwezi wa sita anaidai chadema tshs 600000 na kwamba kina lema walipofika kigoma na chopa hivi karibuni katika ziara yao waliahidi kulipa deni hilo lakini cha kushangaza hadi leo kimya na hakuna kinachoendelea.

Amesema kuwa anashikilia samani za chama hicho ikiwamo viti,meza,bendera na mihuri pamoja na kuitia kufuli hadi atakapolipwa fedha zake na endapo washindwa kulipa hadi mwisho wa mwezi huu atakiburuza chama hicho mahakamani.

hatua ya kushikilia samani imekuja baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na kwamba wale viongozi aliokuwa anawafahamu wamehamia A.C.T Tanzania hivyo ameona njia pekee ya yeye kupata haki yake ni kushikilia mali zao.

my take. Chama kipeleke ruzuku mikoani
"mmechukizwa nilipohoji Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi! siku zote Waasisi wasivigeuze vyama kuwa Mali binafsi " - said arf makamu mwenyekiti chadema
 
acha porojo za uwongo
 
Miaka yote tangu 1995 wamekuwa wakiishi kama digi digi yaani hawakamatiki, lakini kwa sasa UKAWA mmewakamata kisawasawa.

Hongera sana UKAWA, tunasubiri majibu 2015.
 
Kulikuwa na taarifa hapa jana kuwa ofisi ya chadema kasulu pamoja na samani zake imetaifishwa baada ya kushindwa kulipa fedha ya pango.ngoja niitafute niiweke hapa

Habari yako inahusiana nini na uzi huu Ifweero?
 
CHADEMA yashindwa kulipia pango ya ofisi Kasulu
Ofisi ya Chama cha demokrasia na maendeleo jimbo la kasulu mjini inashikiliwa na mwenye nyumba kwa miezi kadhaa hivi sasa baada ya chama hicho kushindwa kulipa kodi ya pango.

Akiongea kwa masikitiko makubwa mmiliki wa jengo hilo (jina limehifadhiwa) ameeleza kuwa hadi mwezi wa sita anaidai chadema tshs 600000 na kwamba kina lema walipofika kigoma na chopa hivi karibuni katika ziara yao waliahidi kulipa deni hilo lakini cha kushangaza hadi leo kimya na hakuna kinachoendelea.

Amesema kuwa anashikilia samani za chama hicho ikiwamo viti,meza,bendera na mihuri pamoja na kuitia kufuli hadi atakapolipwa fedha zake na endapo washindwa kulipa hadi mwisho wa mwezi huu atakiburuza chama hicho mahakamani.

hatua ya kushikilia samani imekuja baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na kwamba wale viongozi aliokuwa anawafahamu wamehamia A.C.T Tanzania hivyo ameona njia pekee ya yeye kupata haki yake ni kushikilia mali zao.

my take. Chama kipeleke ruzuku mikoani
"mmechukizwa nilipohoji Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi! siku zote Waasisi wasivigeuze vyama kuwa Mali binafsi " - said arf makamu mwenyekiti chadema
Acha uongo wa kitoto ofisi imehamia mtaa wa Kagunga mwezi jana, na malipo ya pango yamefanyika ya miezi sita. Uhalisia ni kwamba ofisi za CDM zamani zilikuwa kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa CDM Bw Rajab Bujoro na hakuna malipo aliyokuwa akikidai chama ilikua hisani tu. Sasa ameamua kupangisha nyumba yake kwa biashara kuwa ZAHANATI, jambo ambalo sababu anazijua mwenyewe. Propaganda za kitoto peleka CCM.
 
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umekuwa tatizo kuu linalo isumbua CCM kiasi cha kuanza mikakati kudhoofisha jitihada zinazofanywa na umoja huu kivyovyote vile hata kwa kufanya makosa ya jinai, imefahamika mjini hapa. Hii imetokana na ukweli kuwa umoja huo umeonyesha taa ya kijani kwa mafanikio ya kuiondoa CCM madarakani, hivyo kila upande unaoonekana kuhusika na UKAWA kufanyiwa kila aina ya hila. Jinai hizo ni pamoja na kushusha bendera za CHADEMA na NCCR MAGEUZI na kuzichoma moto.

Hali imezidi kuwa mbaya zaidi hapa Kasulu Mjini juzi baada ya kuwasili kwa Mh. Moses Machali ambaye ni Mbunge wa Jimbo hili la Kasulu Mjini, NCCR MAGEUZI akitokea Bungeni Dodoma ambapo alikuwa akihudhuria kuwawakilisha wananchi wa Kasulu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh. Moses Machali mbali na kuwa Mbunge pia ni waziri kivuli wizara ya UCHUKUZI akiwakilisha kambi rasmi ya upinzani bungeni, na pia ni Naibu Katibu Mkuu NCCR MAGEUZI TAIFA chama ambacho ni wadau wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Hii imemuongezea maadui mamluki wanaopandikizwa na CCM ili kudhoofisha jitihada zake za mapambano dhidi ya serikali dhalimu ya CCM. Muda mfupi kuanzia sasa ikifika saa 9:00 alasiri atakuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kasulu Mjini katika ukumbi wa COmmunity Centre. Kuna tetesi kuwa agenda kuu ni SERIKALI YA CCM HAITAKIWI IONDOLEWE MADARAKANI, SERIKALI TATU HAZIEPUKIKI, na WAJIBU NA UMUHIMU WA WAFANYABIASHARA KWA MAENDELEO YA KASULU NA TAIFA KWA UJUMLA.

Ujio huu wa Moses Machali umekumbwa na changamoto ya mamluki kushusha bendera iliyokuwa Stand ya Taxi Kasulu Mjini jana jioni. Hivi karibuni ilishushwa ya CHADEMA iliyokuwa Standi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani shughuli ambayo inaratibiwa na UVCCM Kasulu na kutekelezwa na baadhi ya vijana wa kijiwe cha waendesha bodaboda Stand Kuu ya Taxi Kasulu Mjini. Ninawasikitikia ukiwaangalia ni wasakatonge, mguu nje mguu ndani watakuja kujuta kushusha bendera hizo ambazo walizichoma moto.

Hali hiyo inasababishwa na ukweli kwamba hapa Mjini Kasulu hakuna vyama pinzani pasua kichwa kwa CCM kama CHADEMA na NCCR MAGEUZI, hivyo basi kwa kuwa kinafasi ya ubunge Moses anaonekana kuwa ndiye ana nafasi kubwa mpaka sasa ya kurudi Bungeni 2015 wanaendesha hila hizo kukwamisha jitihada za muungano wa UKAWA ukizingatia CCM wanawasiwasi ikiwa UKAWA watasimamisha mgombea ubunge mmoja na kumuunga mkono, Kasulu mjini lazima atakuwa Mh.Moses Machali. Hii inawapasua kichwa CCM hawalali. Mbali na kikao hicho cha ndani Jumamosi tarehe 05/07/2014 atakuwa na mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya stand ya taxi Kasulu Mjini.

VIVA UKAWA, VIVA MACHALI ALUTA CONTINUA.
Mh. Moses Machali ninayemfahamu vizuri kiutedaji wake wa kazi, ni mtu shujaa, mpiganaji wa ukweli, mzalendo na asiyeogopa mtu kwa status yake kivyovyote alivyo ilimradi tu anaonekana amekosea na inamlazimu Machali kufyatuka na kumchana live bila chenga. Hii haijalishi ni waziri mkuu, spika wa bunge au naibu uwe mkurugenzi au mwenyekiti wa halmashauri ndiyo kabisaaa ukileta fyongo utajuta kwa nini ulifanya fyongo hiyo katika halmashauri ya Kasulu mjini.

Huwa namkumbuka driver mmoja wa malori ya mizigo kutoka Dar kuja Kasulu, siku moja nikiwa naangalia naye Bunge kwenye TV Mh. Machali alikuwa akichangia hoja ya KUBANA MATUMIZI YA SERIKALI akielekeza fedha za mahitaji yasiyo ya lazima zipelekwe kwenye miundo mbinu ya maji, afya nk. Aliishauri serikali kuwa kulingana na ufinyu wa bajeti na wananchi hawana maji vijijini, ni vema fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya halaiki (sherehe za kiccm) zihamishwe zipelekwe kwenye huduma muhimu kama maji na afya. "...mtu akiacha kuangalia michezo, gwaride, mashairi, ngoma hawezi kufa lakini mtu akikosa maji safi na salama au huduma ya afya anakufa, naishauri serikali izialocate fedha hizo za halaiki zikatengeneze miundo mbinu ya maji na afya...." Aliongeza Mh. Moses Machali.

Kinachonifanya hapo nimkumbuke Driver niliyemtaja ni pale aliposimama kwa mzuka akishangilia na kusema siku zote wabunge wa CHADEMA ni majembe kweli kweli "...umemsikia huyo mbunge wa CDM anawashauri maccm lakini hayaelewi yani kitu ni rahisi mfano ukiacha kuangalia sinema haufi, ukiugua ukakosa tiba au maji safi na salama kifo kinakukumba..." Alisisitiza. Nilicheka kidogo harafu nikamwambia huyo ndiye Mh Moses Machari mbunge wa NCCR MAGEUZI Kasulu Mjini sio wa CDM, akasema hakika mbunge wenu ni jembe, "... huwa ninamfananisha na akina Mnyika, Lema, Ezekiah Wenje na wabunge wengine wa CDM" Aliongeza rafiki huyo from Dar.

Nilimsimulia kazi anazofanya hapa Kasulu kuwabada viongozi wa halmashauri akakumbuka kuwa alishasoma kwenye gazeti moja kuwa nusura ashikane mashati na mkurugenzi kutokana na uchakachuaji wa mali ya Umma. Nikamwambia ninafurahishwa na utendaji wake wa kazi kwani haogopi mtu na amekuwa akiwabana kiasi cha kumchukia. rafiki huyo akaniambia "UKIONA MKURUGENZI,MBUNGE,MWENYEKITI HALMASHAURI NA MKUU WA WILAYA WANAELEWANA UJUE WOTE NI MAFISADI WANAWANYONYA WANANCHI NA UKIONA MBUNGE HAELEWANI NAO UJUE DHAMBI YA UNYONYAJI WANAYOIFANYA MKUU WA WILAYA, MKURUGENZI NK HAPENDEZWI NA ANAICHUKIA NA KUWAKEMEA NA HIVYO LAZIMA WAMCHUKIE NA KUMTENGENEZEA FITINA. KASULU MNA JEMBE MPENI USHIRIKIANO UKOMBOZI HAUJI KWA KUBADILIBADILI WAPAMBANAJI" Mh. Moses Machali anastahili pongezi.
 
Back
Top Bottom