ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Acha wivu wa kike!! Yeye hana haki ya kuwa mwanachama.
Inaonekana hii dhana ya uanachama wa chama cha siasa na utumishi wa uma hujaelewa bado miiko yake.
hata avatar yako imekaa kitubiotubio........uzi wa kinafiki na kuunga unga...mara mazishi, mara uchaguz wa mwenyekiti, mara kufyeka mahindi...uelewek kama unga wa ngano,,,,,maandaz wewe, chapati wewe, mara mkate, vishet.....kajipange uje na kimoja.......
Jambo lolote linapozua maswali mseto elewa lazima kutakuwepo majibu yenye kutofautiana . Ndio maana katika kiswahili zipo tungo tata, kama una zaidi ya hayo tueleze acha hasira usisomeke kiliberali.hata avatar yako imekaa kitubiotubio........uzi wa kinafiki na kuunga unga...mara mazishi, mara uchaguz wa mwenyekiti, mara kufyeka mahindi...uelewek kama unga wa ngano,,,,,maandaz wewe, chapati wewe, mara mkate, vishet.....kajipange uje na kimoja.......
Mod tuondolee huu ushuzi hapa pls
Mwenyekit wa tawi kwanini asizikwe na chama chake ?
Ni mtumishi wa Mahakama naomba kujua ikiwa anapaswa kuwa kiongozi wa chama cha siasa. Haya ni yaliyojiri kwenye mazishi sio maoni yangu. Hebu fikiria ilifika wakati baadhi ya waliohudhuria kuona vile wakaondoka hawakushiriki kuzika. Hivyo basi kama una maelezo ya kisayansi ya sheria ya utumishi wa umma tusaidie kujua tudumishe mshikamano. Habari za ushuzi mnazijua ninyi waliberali hapa ni hoja kwa kwenda mbele!
Jambo lolote linapozua maswali mseto elewa lazima kutakuwepo majibu yenye kutofautiana . Ndio maana katika kiswahili zipo tungo tata, kama una zaidi ya hayo tueleze acha hasira usisomeke kiliberali.
Tarehe 25 Desemba 2013, aliyekuwa karani muajiriwa wa mahakama ya wilaya Kasulu ndugu Joseph Obed Kasyome, alitutangulia mbele za haki. Leo hii imefanyika ibada ya kuzikwa kwake iliyoambatana na mbwembwe nyingi, za kufunika jeneza la marehemu kwa bendera za chama cha mapinduzi, green guard wakaubeba mwili wa marehemu kuelekea kaburini wakati huo huo bendera za CCM zikipepea full mlingoti kwenye vijiti zilipopachikwa.
Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na mkuu wa wilaya Kasulu bw. Dann Makanga,sambamba na Dann Nsanzugwanko, mwenyekiti wa CCM Kasulu Bw. Kaloba na mfiwa (dada wa marehemu) Ester Obed Kasyome, diwani viti maalumu CUF, ilisomwa katika historia fupi ya marehemu kuwa pamoja na yeye kuwa mtumishi wa mahakama pia alikuwa kada na mwenyekiti wa tawi mojawapo la CCM mtaa wa Murubona. Miongoni mwa maswali yaliyoibuka ni je, kuna uhalali mtumishi wa mahakama kuwa kiongozi wa chama cha siasa?
Pia waliohudhuria mazishi hayo walikuwa na viulizo kibao ikiwa mtindo huu wa mbwembwe za namna hii ukiendelea si utakua chanzo cha kubaguana? Chadema watafanya kivyao, NCCR kivyao na kwa kuwa tayari siasa za kibongo zimekuwa uhasama huenda itahatarisha uhusiano wa watanzania na mshikamano wao kupelekea kila jeneza linalopambwa kwa bendela ya chama fulani wazikane wao kwa wao.
Watu waliohudhuria mazishi hayo wengine walifika mbali zaidi, wakasema mbwembwe hizo ni kumufurahisha diwani viti maalumu Ester Kasyome CUF kwa tendo la fadhila alizowafadhili CCM akapokea rushwa kwenye uchaguzi wa nani awe mwenyekiti wa halmashauri ya kasulu katika uchaguzi uliopita wa 2010 na kura yake kumpatia Bw. Lutuli mwenyekiti wa sasa (ccm). Inasemekana kuwa kuna ushahidi wa 100% kuwa diwani huyo wa CUF ndiye alisalilti wanakasulu wapenda mabadiliko ya kidemokrasia.
NB. Dann Makanga ndiye huyo ambaye hivi karibuni amesemwa sana Bungeni kwa kuamuru kufyekwa mahindi ya wakulima na kuwaacha wafugaji wakivunja sheria hiyo hiyo hata Kamanda freeman Mbowe alimtaja. Na
Hivi ujuwe ktk hili jukwaa....hatuna sababu ya kuleta yenye mistari miwili ambayo aina kichwa wala miguu....uwezi kuja uzi wa sentesi mbili wenye mada zaidi ya mbili.....hili ni jukwaa na watu wenye weledi na kujadili mambo tunafikir yanaweza kuleta chachu ya maendeleo katika taifa hili..habari nyembamba kama yako ipeleke kule Fb....watu wanalike kila status.......no arguments .......hivi hukuona neno lingine zaidi kulitumia kiliberali.......????mimi kwa elimu yangu ndogo...niliyosomea watu....huwa naamini mtu mwenye kutamkatamka kitu bila mtu kuanzisha ana mausiano makubwa na hilo neno......."there are no empty term"......acheni hizo mambo...msikurupuke
kwa hoja hapa......!!!
Haa! haa! teh teh! unasema mwenyewe una Elimu ndogo, huo weledi wa kujua watu utaupataje? Tuache wenye Elimu kubwa tunamuelewa vizuri mleta thread hii sio mistari miwili kama ulivoiona kwa Elimu yako duni. We ni mliberali tu au nimuombe Mh. Wenje akufafanulie? Au Mh. Lissu akupashe! Au Mh. G. Lemma akufundishe upate Elimu kubwa? Stay tuned I will be back.
Umekurupuka......tena kama ulkuwa unaoga nje...elimu yangu ni yule mwenye kunufaika nayo...ndio atasema kubwa si mm...mimi bado nataufuta elimu mpk mwisho.....hata level niliyofikia....na kwa upungufu wako na uwezo wako mdogo...uko sahihi kuwa na reference ya wenje na Lema... are they your role models kwa sababu ya ubunge au uchama? reference ya mtu ndio inanifanya kujua kiwango chako cha kufikir....peleken hoja zenu huko fb sio humu....sio mmnakuja na thread hazina kichwa wala miguu hoja za kujadili na wake zenu jikon mnaleta humu.......nilijua mtu kwa kujibu kuhusu uliberi kuna mtu mwingine mwenye kuguswa kama utakuja faster.....!!!MLIIBERI MKUBWA WEWE!!! i have to spend my time wisely sio na wakimbiz wa nchi hii
Chonde chonde, Baba Wawili na Ismaili Mkimbizi acheni kutoka nje ya mada, kama uliberali ndiyo imeleta utata nafuta kauli niliyeitamka. Naombeni mjibu maswali yafuatayo;
1. Mtumishi wa mahakama ya Wilaya (karani) aliyeajiriwa na anakula kodi ya wananchi anaruhusiwa kisheria kuwa kiongozi wa chama cha siasa?
2. Ni vizuri inapendeza kiongozi wa shina , tawi kuzikwa kwa mbwembwe na jeneza limefunikwa kwa bendera za chama CCM Green Guard nao kuubeba mwili wa marehemu na kuwazuia wananchi wa kawaida wasiguse jeneza? Kama ndiyo au sio hebu jengeni hoja.
3. Inaleta picha gani palipo viongozi wa ngazi ya juu wilayani CCM na Serikali na dada wa marehemu ni diwani kukosa idadi kubwa ya watu ukilinganisha na msiba mwingine wa jirani mtoto mdogo aliyefariki na kusindikizwa na watu wengi zaidi ya huyo mtumishi?