ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Tarehe 25 Desemba 2013, aliyekuwa karani muajiriwa wa mahakama ya wilaya Kasulu ndugu Joseph Obed Kasyome, alitutangulia mbele za haki. Leo hii imefanyika ibada ya kuzikwa kwake iliyoambatana na mbwembwe nyingi, za kufunika jeneza la marehemu kwa bendera za chama cha mapinduzi, green guard wakaubeba mwili wa marehemu kuelekea kaburini wakati huo huo bendera za CCM zikipepea full mlingoti kwenye vijiti zilipopachikwa.
Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na mkuu wa wilaya Kasulu bw. Dann Makanga,sambamba na Dann Nsanzugwanko, mwenyekiti wa CCM Kasulu Bw. Kaloba na mfiwa (dada wa marehemu) Ester Obed Kasyome, diwani viti maalumu CUF, ilisomwa katika historia fupi ya marehemu kuwa pamoja na yeye kuwa mtumishi wa mahakama pia alikuwa kada na mwenyekiti wa tawi mojawapo la CCM mtaa wa Murubona. Miongoni mwa maswali yaliyoibuka ni je, kuna uhalali mtumishi wa mahakama kuwa kiongozi wa chama cha siasa?
Pia waliohudhuria mazishi hayo walikuwa na viulizo kibao ikiwa mtindo huu wa mbwembwe za namna hii ukiendelea si utakua chanzo cha kubaguana? Chadema watafanya kivyao, NCCR kivyao na kwa kuwa tayari siasa za kibongo zimekuwa uhasama huenda itahatarisha uhusiano wa watanzania na mshikamano wao kupelekea kila jeneza linalopambwa kwa bendela ya chama fulani wazikane wao kwa wao.
Watu waliohudhuria mazishi hayo wengine walifika mbali zaidi, wakasema mbwembwe hizo ni kumufurahisha diwani viti maalumu Ester Kasyome CUF kwa tendo la fadhila alizowafadhili CCM akapokea rushwa kwenye uchaguzi wa nani awe mwenyekiti wa halmashauri ya kasulu katika uchaguzi uliopita wa 2010 na kura yake kumpatia Bw. Lutuli mwenyekiti wa sasa (ccm). Inasemekana kuwa kuna ushahidi wa 100% kuwa diwani huyo wa CUF ndiye alisalilti wanakasulu wapenda mabadiliko ya kidemokrasia.
NB. Dann Makanga ndiye huyo ambaye hivi karibuni amesemwa sana Bungeni kwa kuamuru kufyekwa mahindi ya wakulima na kuwaacha wafugaji wakivunja sheria hiyo hiyo hata Kamanda freeman Mbowe alimtaja. Na