Kasoro kubwa ya muungano wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasoro kubwa ya muungano wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wakuziba, Jun 25, 2012.

 1. w

  wakuziba Senior Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano iliopo sasa, mtu yeyote ambaye amezaliwa ktk eneo la jamhuri ya muungano baada ya muungano, ni raia halali wa jamhuri ya muungano. ana uhuru wa kuishi na kufanya kazi ktk jamhuri bila kubaguliwa. wapemba wengi mnaowaona huku bara, wengi wao wamezaliwa baada ya muungano tena huku bara. ni watanzania wenye haki ya kuishi huku bara. ni kabila kama mmakonde, mnyamwezi, mzaramo nk... wanakua raia wa jamhuri ya muungano wa tanzania automatically. ktk vituo vya polisi na mahakamani, wakiulizwa kabila wanasema mpemba. Kwa upande wa zanzibar, mtu kutoka bara ana uhuru wa kufanya kazi na kuishi znz lkn hawezi kuwa raia hadi aishi muda usiopungua miaka kumi kisha auombe urai.


  hawa wapemba wanaoishi bara, wengi wao (asilimia kubwa) hawana uraia wa zanzibar. hawaruhusiwi kupiga kura znz. wakienda wanaenda kutembea kama mmakonde anavyo tembea znz. tofauti ni kuwa wapemba wa bara wana ndugu zao na hata wazazi wao znz. ukifuatilia takwimu, utaambiwa wazanzibari hawazidi 1.5 milion. hawa ni wazanzibari wakazi wa unguja na pemba walio na vitambulisho vya uraia / makazi. znz ni wajanja. wanajua kuwa hata muungano ukivunjika, chain yao ya wapemba zaidi ya milioni 4.5 ipo huku bara na ni raia halali. kama ni kosa basi lilifanyika mwanzoni zilipoundwa kanuni za muungano. kufuta tanganyika kuliwapoteza wamakonde, wahaya, wahehe ....nk


  iwapo kama tutavunja muungano, kisheria, wapemba watakua na haki ya kuendelea kuishi bara kama kabila mojawapo la tanganyika. Wana haki sawa na mmakonde, mnyamwezi, mzaramo nk... huu ndiyo ukweli kisheria. Kuna watu wanadhani kuwa nyumba za wapemba zilizotapakaa huku bara na maduka yao mengi vitataifishwa.

  TANBIHI
  1- m2 anaweza kutoa mfano wa sudan. muungano wetu haufanani na kadhia ya sudan.
  2- vilevile hatufanani na muungano wa ulaya. kule kila nchi inatambulika. hapa kwetu tuliiua tanganyika na kufanya wapemba wawe kabila mojawapo la tanganyika.
  F
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii isikupe hofu, ikitoke wakataka kuvunja muungano NK, watachagua wanakotaka, kama ilivyokuwa wakati wa uhuru.
   
Loading...